" WANANCHI YATUMIENI MAONYESHO YA NANENANE KUJIFUNZA MBINU BORA ZA KILIMO - RC CHACHA

WANANCHI YATUMIENI MAONYESHO YA NANENANE KUJIFUNZA MBINU BORA ZA KILIMO - RC CHACHA

Na Lucas Raphael,TaboraMkuu wa mkoa wa Tabora ,Paulo Chacha amewataka wananchi Kuyatumia maonyesho ya nane nane kujifunza mbinu Bora za uzalishaji wa mazao ya Kilimo,Mifugo na uvuvi kupata maarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya uzalishaji wenye tija ili waweze kujikwamua kiuchumi .Kauli hiyo ilitolewa jana   wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya nane nane kwa Kanda ya Magharibi yaliyofanyika katika viwanja vya Ipuli  mkoani Tabora.Chacha alisema kwamba maonyesho hayo yalitumika vizuri yanaweza keta Tija kwa wakulima na kuweza kuongeza uzalishaji mkubwa."Wengi wetu tupo kwa lengo la kuona kujifunnza mbinu Bora , uzalishaji mazao ya Kilimo ,mifumgo na uvuvi ili kupata maarifa yatakayotusaidia kupiga hatua kwenye Mapinduzi ya kijani na hivyo kuinua Pato na uchumi kwa Kaya zetu na taifa kwa ujumla " alisema Chacha.Kwa upande wake , Msajili wa Mamlaka ya Wanunuzi wa Mbegu kutoka Wizara ya Kilimo Twalib Njohole alibainisha lengo la maonyesho ya nane nane ni kutoa elimu na teknolojia bora ya kilimo ili kuongeza uhakika wa uzalishaji wa mazao.Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Okia John, aliwataka Wakulima kutumia Mbegu ambazo zimethibitishwa na mdhibiti ubora ili waweze kupata mavuno bora ."Tuna mhakikishia Mkulima Mbegu ambayo tunampa hapa kwenye hili banda atakapofika ni Mbegu bora kwa sababu imethibitisha na mdhibiti ubora wa Mbegu" Okia alisisitizaMaonyesho ya nane nane kwa Kanda ya magharibi yanafanyika kwenye viwanja vya Ipuli ambapo tamati yake itakuwa Agosti 8,2025 ambapo yatafungwa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Saimon Silo."maonyesho haya yamebebwa na kauli mbiu ya " _Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"._Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post