Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole mkoani Mbeya Dkt. Tulia Akson ameeleza sababu za kwanini wananchi wa mkoa wa Mbeya wanakwenda kumpa kura za kishindo na za heshima mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dokta. Samia Suluhu Hassan
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo septemba 4, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Old Airport) mkoani Mbeya.
Dkt. Tulia amesema safari hii wana Mbeya wamekubaliana kumpa Rais Samia kura sio tu za ushindi lakini ushindi wa heshima kutokana na kuituliza Mbeya kwani Mbeya ya sasa haina maandamano wala fujo bali nguvu kubwa imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo hali iliyowafanya vijana mkoani humo kuwa na shughuli za kufanya.
"Mhe Rais kwa nini wana Mbeya tumekubaliana kukupa kura sio tu za ushindi lakini ushindi wa heshima umefanya makubwa hasa katika sekta ya Afya ambapo hapa Mbeya mjini tumepata zaidi ya shilingi Bilioni 20 lakini hospitali yetu ya rufaa ya kanda inazo mashine zile ambazo zamani walikuwa wanafuata huduma Dar es salaam sasa huduma zinatolewa hapa kutokana na uwepo wa vifaa tiba ulivyovileta Mhe nasema safari hii tutakuheshimisha"alisema Dkt Tulia.
Akizungumzia upande wa sekta ya Elimu amesema wamefanikiwa kupata zaidi ya shilingi Bilioni 31.1 ambapo shule mpya za msingi na mpya za sekondari zimejengwa huku vijana wa mkoa huo wakipata mikopo.
Dokta Tulia amesema katika eneo la maji Mbeya Jiji ambalo ni Jiji pekee nyanda za juu kusini limekuwa na changamoto ya maji ambapo Bilioni 30 zimeletwa kuondoa changamoto hiyo huku akiipongeza mamlaka ya maji kwa kutumia vizuri shilingi Bilioni 16 kutoka kwenye mapato ya ndani kwani miradi mbali mbali inaendelea na kata mbali mbali kati ya kata 36 za Jimbo la Mbeya mjini zimepata huduma ya maji sasa.
Amesema kuwa kuna miradi mikubwa inayokwenda kumaliza tatizo la maji ambapo pia zimeletwa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 21.7 .
Ameongeza kuwa stendi ya mabasi ya mkoa wa Mbeya inajengwa pia ili kuwaondolea wananchi changamoto huku ikiwa ni moja ya eneo hilo kuwa kitovu kikubwa cha biashara.
Mhe Tulia ameongeza kuwa katika kata ya maendeleo zaidi ya shilingi bilioni 6 zinajenga jengi la ghorofa kwa ajili ya soko jipya.
"Uwezo tunao Dokta Samia nakuahidi utafurahi tutakuheshimisha alisema Dkt Tulia.
Aidha ameishukuru Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kulipongeza kwa kazi kubwa iliyofanyika chini ya mkurugenzi na viongozi wengine waliohakikisha mikopo ya asilia 10 inatoka kwa wakati ambapo vijana wanawake, watu wenye ulemavu zaidi ya 3,000 wamepewa mikopo ya zaidi ya Bilioni 7 kutokana na mapato ya ndani kama agizo la Mhe Rais linavyosema.
Katika upande wa miundombinu ya Barabara ya njia nne yenye kilometa 218 kuanzia Igawa mpaka tunduma inajengwa, barabara za lami zimejengaa, madaraja yamejengwa, na Barabarani korofi zinakarabatiwa.
Mgombea ubunge huyo kwa niaba ya wananchi amemshukuru Rais Samia kwa neema aliyoitoa kwa wananchi wakulima wa Uyole kwa ruzuku ambayo Dokta Samia ameweka kwa ajili ya pembejeo ya kilimo ikiwa ni pamoja na mbolea ambayo imewafanya watoke hatua moja kwenda nyingine kwani kiasi cha fedha walichokuwa wakitoa kwenye mbolea kwani wamepunguziwa bei.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment