Na Mwandishi Wetu.Mradi wa MOWADITA-SHINYANGA umeendelea kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia utekelezaji wa shughuli za utetezi wa haki na ushawishi kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu, sambamba na mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi hayo.Katika mdahalo ulioandaliwa hivi karibuni, washiriki wamepata uelewa mpana kuhusu haki zao za msingi, ikiwa ni pamoja na namna ya kuzitumia vyema fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii ili kujiendeleza kiuchumi na kijamii.Akizungumza katika mdahalo huo, mmoja wa wawezeshaji alisema hatua hiyo imeongeza mwamko wa wanawake na wasichana wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao.Aidha, washiriki wameelimishwa juu ya mikataba ya kimataifa, sheria, sera na miongozo inayogusa upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu, jambo ambalo limeongeza ujasiri wao wa kudai haki katika maeneo wanayoishi na kufanyiwa kazi kwa masuala yanayowahusu.Mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa nayo yameelezwa kuongeza uwezo wa wanawake na wasichana hao kuanzisha na kuendeleza miradi midogo ya kiuchumi ili kujipatia kipato na kujitegemea.Mradi wa MOWADITA-SHINYANGA unaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha wanawake na wasichana wenye ulemavu wanakuwa sehemu ya maendeleo endelevu katika mkoa wa Shinyanga.Pamoja na mambo mengine Taasisi ya Mowadita SHINYANGA imeweza kujenga mahusiano baina ya Wanawake na wasichana wenye ulemavu na kuwawezesha kuunda vikundi vitano vya Wanawake na wasichana wenye ulemavu ambavyo ni KIKUNDI CHA AMANI, TUPENDANE , UPENDO, COMMUNITY BASED ORGANISATIO ( CBO) NA UKOMBOZI kwa lengo la kuwaweka pamoja na kufanya shughuli za ujasiriamali2. MABADILIKO-Wanawake na wasichana wenye ulemavu wameweza kuungana na kuweza kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutatua changamoto zao.Vikevile Taasisi ya MOWADITA - SHINYANGA kuona mabadiliko ambapo Wanawake na wasichana wenye ulemavu wameweza kuungana na kuweza kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutatua changamoto zao.-Wanawake na wasichana wenye ulemavu wameweza kutoa hofu na sasa wanaweza kufika ofisi mbalimbali kutafuta namna ya kutatua changamoto zao ikiwa ni pamoja na pia baadhi wameweza kupata ujasiri wameweza kushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi *mkuu* .Pamoja na hayo Taasisi ya MOWADITA -SHINYANGA imekumbana na changamoto katika utekelezaji wa mradi ambapo-Baadhi ya washiri wenye ulemavu wa UZIWI kutofahamu lugha ya alama ya kitaifa na badala yake kuwa na ufahamu wa lugha ya alama ya kienyeji hivyo kufanya mawasiliano baina yao na mkalimani wa lugha ya alama kuwa magumu.-Na changamoto nyingine ni kupokea fedha pungufu kwa baadhi ya shughuli tofauti na bajeti tuliyoiandaa kutokana na kushuka kwa thamani ya Dola wakati wa ingizo la fedha hizo na kupelekea kupunguza baadhi ya gharama za uendeshaji wa shughuli za mradi kulingana na mahitaji.TUMEJIFUNZA NINI? -Wanawake wengi wenye ulemavu Bado wanaishikatika hali ya maisha ya ukatili na unyanyasaji. -Bado Kuna Wanawake na wasichana wengi wenye ulemavu ambao hawajui Haki zao na hatukuweza kuwafikia . -Mradi tunaoendelea nao ni mdogo ukilinganisha na ukubwa wa changamoto za Wanawake na wasichana wenye ulemavu .

Post a Comment