" BOMU LA KUTEGWA LAONDOA UHAI WA WA JENERALI WA URUSI.

BOMU LA KUTEGWA LAONDOA UHAI WA WA JENERALI WA URUSI.

Na:Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Mkuu wa Kurugenzi ya Mafunzo ya Uendeshaji katika Jeshi la Urusi, Luteni Jenerali Fanil Sarvarov, ameuawa baada ya bomu lililotegwa chini ya gari lake kulipuka kusini mwa Moscow.

Msemaji wa Kamati ya Uchunguzi, Svetlana Patrenko, amesema mapema leo kuwa Jenerali Sarvarov alifariki kutokana na majeraha aliyopata, na kwamba uchunguzi rasmi tayari umeanzishwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, mlipuko huo ulitokea majira ya saa moja asubuhi katika eneo la maegesho ya magari kwenye mtaa wa Yaseneva, Moscow, wakati Sarvarov akiwa ndani ya gari.

Post a Comment

Previous Post Next Post