Tunaposhuhudia viongozi kama Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakisema "tunafanya tathmini ya kina kabla ya kuanza safari," tunapaswa kushukuru. Ni rahisi kisiasa kuruhusu treni ipite ili kufurahisha watu, lakini ni uungwana wa kitaaluma kusimamisha safari ili kulinda roho za watu.
Treni moja ya SGR inaweza kubeba hadi abiria 1,000. Kujaribu kupitisha treni kwenye njia ambayo haijahakikiwa baada ya mvua kubwa ni kucheza na maisha ya watu elfu moja.
Shirika la reli nchini,TRC inafuata taratibu za kimataifa za "Safety First" (Usalama Kwanza). Udaku wa mitandaoni mara nyingi haujui gharama za kurekebisha ajali ya reli au thamani ya maisha ya binadamu, wakilenga kubadilisha ukweli kuwa ya chuki katika vichwa vya watu.
Usalama wa reli hauna mbadala. Hatua inayochukuliwa na serikali ya kukagua njia kutoka Morogoro hadi Dodoma ni ya kishujaa na ni ya lazima kwa mujibu wa kanuni za usafirishaji duniani.
Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa reli ya kisasa ipo salama na shirika litaendelea kuchukua tahadhari zote kwa ajili ya usalama wa abiria wanaotumia huduma hiyo ambapo kwa sasa tathmini ya kina inafanyika ili kujiridhisha na hali ya njia.
Akihitimisha maelezo ya mawaziri walioambatana naye kwenye ziara ya siku moja,kukagua uharibifu uliosababishwa na mafuriko mkoani Morogoro, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema jambo linalofanywa na TRC kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi ni la msingi ili kujiridhisha na hali ya usalama wa reli hiyo.
Usalama wa reli duniani kote haufanyiwi mzaha na TRC nayo haifanyi mzaha kwani usalama huu unahusisha mifumo migumu ya kiufundi inayobeba maelfu ya abiria na maelfu ya tani za mizigo kwa wakati mmoja.
Inapaswa kueleweka kuwa TRC si shirika la kwanza kusimamisha treni kufanya ukaguzi kwani mataifa yaliyoendelea kama Japan, Uingereza na China hufanya hivyo mara kwa mara pindi hali ya hewa inapochafuka ili kuzuia majanga makubwa.
Usalama wa reli unategemea utengamano wa njia ambapo maji ya mvua yanaweza kulainisha udongo wa chini na kusababisha reli kupoteza uwezo wa kubeba uzito wa treni bila kuonekana kwa nje. Aidha mifumo ya kielektroniki ya mawasiliano na nyaya za umeme wa msongo mkubwa zinahitaji ukaguzi wa mara kwa mara ili kuzuia shoti au hitilafu zinazoweza kusababisha ajali mbaya na ndiyo maana wataalamu hawashauriwi kukurupuka.
Dunia ya leo inapambana na mabadiliko makubwa ya tabianchi yanayoleta mvua zisizotabirika na hivyo taasisi zinazosimamia usafiri wa reli lazima ziwe makini zaidi kuliko wakati wowote ule.
Na ndio maana hatua ya serikali kuelekeza nguvu kwenye ujenzi wa mabwawa kuwezesha udhibiti wa maji ni hatua ya kisayansi ya kuzuia maji huko yanakotokea kabla hayajaleta madhara kwenye tuta la reli , hatua hii ni jambo linaloonyesha weledi wa hali ya juu la utaalamu kwa wasimamizi wa reli na treni.
Tuache kusikiliza udaku wa mitandaoni usiofikia kichwa wala kujua hatari zilizopo katika uendeshaji wa reli za kisasa kwani usalama wa reli hauna mbadala na hautakiwi kufanyiwa majaribio ya kisiasa.
Hakika kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda miundombinu hii ya mabilioni ya fedha ni ya kupongezwa na inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania anayethamini uhai na maendeleo ya taifa lake.
Mifano ya Kimataifa: TRC si ya Kwanza na si ya Mwisho
Duniani kote, mashirika makubwa ya reli yanayoheshimika husimamisha huduma mara moja pindi hali ya hewa inapochafuka au hitilafu inapohisiwa:
Japan (Shinkansen): Licha ya kuwa na teknolojia ya juu zaidi duniani, Shirika la Reli la Japan (JR Group) husimamisha treni zote za mwendokasi mara moja kukitokea tetemeko la ardhi au mvua kubwa zinazovuka kiwango cha usalama. Hawasubiri ajali itokee; wanasitisha safari kwanza, kisha wanakagua njia yote.
Uingereza (Network Rail): Mara nyingi wakati wa msimu wa dhoruba (storms), Network Rail husimamisha safari kote nchini ili kukagua kama kuna miti au vifusi vimeangukia njia. Hawajali malalamiko ya abiria kuhusu kuchelewa, wanajali "Zero Accidents."
China (CRRC): Katika kipindi cha mafuriko makubwa, China imekuwa ikifunga njia za reli kwa siku kadhaa ili kufanya tathmini ya madaraja.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment