" DC SOLOMONI ITUNDA AMUWAKILISHA RC MALISA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE CCT KITAIFA MJINI MBEYA

DC SOLOMONI ITUNDA AMUWAKILISHA RC MALISA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE CCT KITAIFA MJINI MBEYA


Na mwandishi wetuMisalaba Media mbeyaSiku ya Maombi ya Dunia Kitaifa hapa Tanzania kupitia Christian Council of Tanzania (CCT) imefanyika Februari katika ukumbi wa Teofilo Kisanji University (TEKU) jijini Mbeya.Kongamano hilo liliongozwa na Neno Kuu lisemalo:“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo mizito, nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28–30).Ibada ilianza kwa maandamano ya waumini yaliyoanzia Kabwe kuelekea ukumbi wa TEKU. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiroho akiwemo Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Askofu wa Anglican Church of Tanzania Dayosisi ya Southern Highlands, Askofu wa Moravian Church Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi, pamoja na viongozi waandamizi wa CCT.Katibu Mkuu wa CCT, Mchungaji Canon Dkt. Moses Matonya, aliwapongeza washiriki kwa ushiriki wao mkubwa na kuwatambua wanawake kuwa ni “jeshi kubwa” lenye mchango muhimu katika kanisa na taifa.Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomoni Itunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa, aliipongeza CCT kwa kuandaa kongamano hilo mkoani Mbeya na kusisitiza umuhimu wa kufundisha amani, upendo na mshikamano wa kitaifa.Aidha, aliwasihi washiriki kuondoa roho za chuki na kuishi dini safi kwa kuwajali wajane, wagonjwa, wahitaji na yatima.“Baada ya kongamano hili kila mmoja akaiishi dini safi inayompendeza Mungu,” alisema Itunda.Alisisitiza pia kudumisha upendo kuanzia katika familia zetu, huku akitoa wito wa kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake.“Kila mtu aache mizigo mahali hapa kwenye ibada, kila mtu aondoke akiwa mwepesi, tuwe na mabadiliko makubwa kiroho,” aliongeza.Kutokana na ujumbe huo mzito, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Konde alimtunuku DC Itunda heshima ya uzee wa Kanisa na kumkaribisha kuongoza ibada katika moja ya makanisa ya dayosisi hiyo.Kongamano hilo limehudhuriwa na wawakilishi wa Idara za Wanawake CCT kutoka mikoa mbalimbali nchini. Aidha, ibada hiyo iliambatana na uzinduzi wa kitabu cha mwongozo wa Idara ya Wanawake CCT kinacholenga kuimarisha umoja na utendaji wa wanawake ndani ya CCT.Kongamano limeandaliwa na Idara ya Wanawake ya CCT chini ya uratibu wa Mama Askofu Esther Muhagachi.

 


Post a Comment

Previous Post Next Post