Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mhe. Kinjeketile Ngombale Mwiru, ametangaza kugharamia nauli ya kwenda na kurudi kwa wagonjwa pamoja na msindikizaji mmoja watakaokwenda kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kambi maalumu ya upasuaji wa mabusha inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 09 hadi 25 Februari, 2026, katika hospitali hiyo ya rufaa. Kambi hiyo inalenga kuwasaidia wananchi wanaosumbuliwa na tatizo la mabusha kupata huduma ya matibabu kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza kuhusu mpango huo, Mhe. Mwiru amesema kuwa lengo lake ni kupunguza gharama kwa wananchi maskini wa Jimbo la Kilwa Kaskazini na kuhakikisha hakuna mgonjwa anayeshindwa kupata matibabu muhimu kwa sababu ya ukosefu wa nauli.
Aidha, mbunge huyo amewataka wananchi wote wanaohitaji kufanyiwa upasuaji huo kuripoti katika vituo vya afya vilivyotajwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali (check up) ili kuthibitisha kama wanahitaji kufanyiwa upasuaji. Vituo hivyo ni Kituo cha Afya Tingi, Zinga Kibaoni, Kipatimu na Somanga.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment