Madereva wa Magari ya abiria ya masafa marefu wameaswa kuacha kufunga taa za gari zenye mwanga mkali ili kuepuka ajali pindi wanapopishana na watumiaji wa vyombo vingine vya moto barabarani.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amebainisha kuwa tabia ya madereva hao kuwasha taa zenye mwanga mkali zinapelekea watumiaji wengine wa vyombo vya moto kushindwa kuona kilichopo mbele yake na kusababisha kukosa uelekeo hali ambayo inaweza kusababisha ajali pindi wanapopishana barabarani.Aidha Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kuheshimu watumiaji wengine wa barabara na kuacha tabia zinazopelekea kuwa chanzo Cha ajali barabarani.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment