Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Watanzania wameaswa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufikia maendeleo yao badala ya kutegemea serikali kwenye masuala yaliyo ndani ya uwezo wao.
Ushauri huo umetolewa Jijini Mwanza na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Calvary Assemblies of God (CAG) Dk Danstan Maboya alipokuwa akizundua Kanisa la Uzima Tele katika eneo la Nundu kwenye Kata ya Buzuruga lilojengwa kwa zaidi ya milioni 50 kutokana na michango ya waumini wake.
Alisema jitihada za waumini katika kushughulikia masuala ya maendeleo yao ni mhimu katika kufikia kwenye malengo waliyo nayo katika maeneo yao.
Dk Maboya aliwakumbusha waumini wake kutambua kuwa hitaji la kufanya kazi limebainishwa hata kwenye vitabu vitakatifu ambapo Mwenyezi Mungu alisema asiye fanya kazi na asile.
"Masuala ya mila n desturi zetu za kiafrika zisiwe ni kikwazo katika misingi ya imaani zetu" alisema Dk Maboya.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amir Mkalipa, Amos Mzoke alisema wanapongeza juhudi zilizowezesha kujengwa kwa Kanisa hilo kwani kazi zifanywazo na makanisa popote pale huduma zake huwa ni misingi ya amani na utulivu wa nchi.
Alisema wamehamasika kuona jitihada zilizofanywa katika ujenzi wa kanisa hilo hivyo wao kama serikali wameamua kuunga mkono kwa kuchangia shilingi 200,000.
Naye Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza John Kafiti kupitia kwa Katibu wake Magoti Biseko walilipongeza Kanisa hilo kwa kuhamasishana na kuchangia katika ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada.
Alisema kuwepo kwa amani na utulivu ndani ya Tanzania kunachangiwa na vitu vingi ikwemo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Taasisi za dini katika kuhubiri upendo na mshikamano wa watu.
Mchungaji wa Kanisa hilo Samweli Kisinza aliwapongeza waumini wake kwa moyo huo wa kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo kwa jitihada zao wenyewe huku vilevile akipongeza ushirikiano wanaopata toka serikalini.
Alisema kwa sasa wameshatumia zaidi ya shilingi milioni 50 huku wakiendelea na umaliziaji wake katika kuwezesha kanisa kuwa na hadhi nzuri ambapo wanakadiria zaidi ya shilingi milioni 80 zitakuwa zimetumika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment