
Na. OWM – KAM (Rukwa)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametoa siku saba kwa Kampuni ya Tabono Consultant kufika Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Agizo hilo limetolewa kufutia changamoto za kutofuata sheria za kazi hususani kwa wafanyakazi anaowasimamia, zilizoripotiwa na Afisa Kazi wa Mkoa wa Rukwa.
Aidha, miongoni mwa changamoto zilizobainishwa ni kutowasilishwa kwa michango ya wafanyakazi katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kupitia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kupooza Umeme cha Sumbawanga (TAZA), unaosimamiwa na kampuni ya TBEA Co Ltd.
“Tabono Consultant anatakiwa kufika ofisini Jijini Dodoma kuonana na Kamishna wa Kazi kufuatia changamoto za ukiukwaji wa sheria za kazi zilizoripotiwa na Afisa Kazi Mkoa wa Rukwa” amesema.
Mhe. Sangu, ameelekeza wahusika wafike na nyaraka za vyeti vya usajili ili kubaini kama wamesajiliwa rasmi kama mwajiri au msimamizi, na pia wawaslishe vielelezo vya michango ya wafanyakazi (NSSF) na (WCF) pamoja na ripoti ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).
Awali akitoa taarifa kuhusu Tabono, Afisa Kazi Mkoa wa Rukwa Kathbert Kumburu, amesema kuwa mwajiri huyo anatekeleza Amri ya Kima cha Chini cha Mshahara, lakini anakabiliwa na changamoto kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja kama Mwajiri na Wakala wa Ajira.
Pia, amekuwa akikata michango ya NSSF na WCF kwa wafanyakazi bila kuiwasilisha kwa mamlaka husika sambamba na kukatisha mikataba ya wafanyakazi kinyume na sheria.
Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa kampuni ya Tabono, Bi. Fatma Mkwiru, amesema kuwa yeye ni mpya katika nafasi hiyo na kwamba dosari zilizobainika zilifanywa na maafisa rasilimali watu waliotangulia kabla yake. Aidha, ilielezwa kuwa kampuni ya Tabono imekuwa ikiitwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga mara tano ili kufika na kutoa ushirikiano, lakini haikufanikiwa kuitikia wito huo kwa wakati.
Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa Tabono Fatma Mkwiru, amesema yeye ni mpya kazini na kuwa dosari hizo zilifanywa na maafisa rasilimali watu waliopita.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi katika mradi huo, Said Hemed amesema wafanyakazi wamekuwa wakikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao bila kupewa maelezo ya kina kuhusu zinakoelekezwa.
Ameeleza kuwa kiasi kinachokatwa hakilingani na michango inayopaswa kuwasilishwa katika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment