
Watani wa jadi Simba SC na Yanga SC wamefanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Machi 1, 2026, katika Uwanja wa Amani, Visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa, huku Simba SC wakionekana kuwa bora katika kipindi chote cha mchezo.
Kipindi cha pili, Simba SC kupitia mshambuliaji wake, Selamani Mwalimu, walipata bao, lakini refa wa mchezo huo alilikataa kwa madai kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea (offside).
Hadi dakika 90 za mchezo huo, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake, na hivyo kugawana pointi, huku Yanga SC wakiwa wenyeji wa mchezo huo.
Kufuatia matokeo hayo, Yanga SC wanafikisha pointi 29 wakiwa katika nafasi ya kwanza, huku Simba SC wakifikisha pointi 24 katika nafasi ya tatu. Huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 11 kila moja.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment