" Rea yatoa rai kwa wananchi wilayani Butiama kujiunga na huduma ya umeme na matumizi ya nishati safi ya kupikia

Rea yatoa rai kwa wananchi wilayani Butiama kujiunga na huduma ya umeme na matumizi ya nishati safi ya kupikia

 







📌 *Wananchi wapewa elimu ya nikonekt* .


📌 *Wananchi waaswa kutumia nishati safi na salama ya kupikia* .


📍 *Butiama.* 


Wakazi wa wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara,waaswa kutumia nishati safi na salama ya kupikia, kujiunga na huduma ya umeme  pamoja na  kutunza miundombinu ya umeme ili miundombinu hiyo iweze kudumu na  kutoa huduma kwa wananchi kwa  mda mrefu.


Rai hiyo imetolewa leo jumatatu Machi 02, 2026 na wataalamu wa REA na TANESCO walipofika katika wilaya hiyo kutoa elimu na uhamasishaji wa miradi ya nishati vijijini.


Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi amesema,


Kwa sasa taratibu za uombaji huduma ya umeme zimeboreshwa zaidi  na hakuna tena mambo ya kutumia fomu kufanya maombi ambapo kwa kutumia tu namba ya Nida mwananchi anaweza kufanya ombi la  umeme moja kwa moja TANESCO kupitia huduma ya NIKONEKT.


“Kwa kutumia simu janja, mwananchi atapakua huduma ya Nikonekt na kufanya maombi au kama ni simu ya kawaida atabonyeza *152*00# na kisha kufuata maelekezo ya kufanya ombi, hakuna mawakala wanaosajili maombi mtaani tafadhali tuepuke vishoka” mkomi alisisitiza.


Aidha, mkomi ameongezea kuwa, pamoja na umeme kufika majumbani ni vyema wananchi walio eneo la mradi wakachangamka na kutumia fursa  hiyo kujiunga mapema na huduma ya umeme.


Pia, Wakala umefanya Kampeni zinahusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia.


 *Mwisho* .

Post a Comment

Previous Post Next Post