" DIPLOMASIA YA UCHUMI 2026/27: MAMBO YA NJE KUIMARISHA TASWIRA NA MASLAHI YA TAIFA DUNIANI

DIPLOMASIA YA UCHUMI 2026/27: MAMBO YA NJE KUIMARISHA TASWIRA NA MASLAHI YA TAIFA DUNIANI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi mikakati yake ya kuhakikisha kuwa taswira, heshima, na maslahi ya taifa yanazidi kuimarika katika nyanja za kimataifa kupitia vipaumbele vya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2026/27.

 Waziri wa wizara hiyo, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amewasilisha mpango huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama mjini Dodoma, akisisitiza kuwa mwelekeo wa wizara kwa kipindi kijacho utajikita zaidi katika kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje kwa vitendo, hususan kupitia diplomasia ya uchumi. Hatua hii inalenga kuifungua Tanzania zaidi kwa ulimwengu, kuvutia uwekezaji wa kigeni, na kupanua fursa za kibiashara kwa Watanzania ndani na nje ya mipaka.

Katika maelezo yake kwa kamati hiyo, Balozi Kombo amebainisha kuwa mbali na kulinda heshima ya nchi, wizara imejipanga kuimarisha uratibu na ushirikiano wa uwili, kikanda, na kimataifa ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa mshiriki muhimu katika majukwaa ya maamuzi duniani. 

Vipaumbele hivyo pia vinagusa maboresho ya ndani ya wizara, ikiwemo kuimarisha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi, kukuza utawala bora, na kusimamia rasilimali watu. 

Aidha, wizara imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo itakayosaidia taasisi zilizo chini yake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, jambo ambalo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa diplomasia yetu inaleta tija ya moja kwa moja kwa uchumi wa nchi.

Utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa mwaka ujao wa fedha utazingatia miongozo mikuu ya kitaifa na mikataba ya kimataifa inayoinyooshea nchi njia ya maendeleo. Balozi Kombo amesisitiza kuwa mpango huo umefungamanishwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, pamoja na Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/27 - 2030/31). 

Vilevile, utekelezaji huo utazingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025-2030, ambayo inaweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kimataifa kwa ajili ya ustawi wa wananchi na kukuza uchumi jumuishi.

Uwepo wa Tanzania katika jumuiya za kikanda kama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaendelea kuwa kipaumbele cha kwanza katika kulinda soko la ndani na ushirikiano wa usalama. 

Balozi Kombo amefafanua kuwa wizara itahakikisha mikataba ya uanzishwaji wa jumuiya hizo na ajenda za kimataifa kama Ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika zinazingatiwa kikamilifu. Hii itasaidia Tanzania kuendelea kuwa mdau wa kuaminika katika masuala ya maendeleo endelevu na amani duniani, huku ikitumia nafasi hiyo kuvutia wabia wa maendeleo na wawekezaji wa kimkakati katika sekta mbalimbali za uzalishaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Najma Giga, amebainisha kuwa Bunge litaendelea kuisimamia wizara ili kuhakikisha kuwa rasilimali zinazotengwa zinatekeleza vipaumbele vilivyoainishwa kwa ufanisi na weledi. 

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post