Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Waziri wa fedha Balozi Khamis Mussa Omar amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo watahakikisha wanakuza uchumi wa mwanamke mmojammoja na taifa kwa ujumla.Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wananwake katika Sekta ya Fedha Tanzania (TAWIFA) amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua za kisera na kiuchumi kuwawezesha wanawake na vijana wengi kuhakikisha wananufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri zote nchini."Natoa wito kwa taasisi zote za kifedha kuendelea kubuni bidhaa za kuwashawishi wanawake kushiriki masuala ya kifedha, TAWIFA ianzishe vigezo vya kutambua mafanikio kwa kutoa vyeti na tuzo, kuongeza wanawake wawakilishi katika masuala ya fedha na serikali itahakikisha katika bodi za taasisi za fedha wanawake wanashirikishwa kwa asilimia 30" amesema Balozi Khamis.Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Wanawake katika sekta ya fedha Tanzania TAWIFA Bi, Fikira Ntomola amesema wamefanikiwa kumuelimisha mwanamke katika masuala ya fedha ambapo kwa Dodoma na Zanzibar takriban wanawake 800 wamenufaika, Arusha wanawake 200, kuanzisha mafunzo ya elimu ya fedha shule 6 za msingi mkoani Dodoma wanatarajia kuotesha miti 2000 mkoani Arusha."Ni fahari kubwa kuona Watanzania watu wazima76% wakiwemo wenye ulemavu wanatumia huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu kidigitali, ikumbukwe kuwa Dira ya Taifa 2025-2050 inalenga uchumi wenye ubunifu, kustawisha watanzania na kila mmoja mmoja kuchangia uchumi wake na taifa kwa ujumla" ameeleza Bi Fikira.Vilevile Naibu Gavana wa Benki Kuu Sauda Msemo amebainisha kuwa wanawake wanaotakiwa kuwa viongozi lazima waandaliwe kwa kupewa mafunzo maalum ili kuwajengea uwezo wa kujiamini, mtazamo wa kijinsia kuzingatiwa na kuhusishwa katika fulsa."Kutokana na elimu ndogo umiliki wa mali kwa mwanamke bado ni mdogo, jamii bado ina dhana potofu kuwa mwanamke hatakiwi kurithi wala kuzalisha mali"amesema Naibu Gavana Sauda.Katika namna hiyo hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Dkt. Saada Mkuya amesema mpango wa kujenga vyumba vya kunyonyeshea watoto katika masoko umeanza kutekelezwa ili kudumisha maadili mema katika jamii."Tukumbuke kuwa ili mwanamke awe na furaha na afya njema ya akili ni lazima watoto wake wawe na afya njema bila changamoto yoyote katika ukuaji wao sambamba na hayo tunatakiwa kuwashirikisha wanaume kikamilifu kwa sababu wanawake bila wanaume hawawezi".SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment