" Simba SC yaingia ubaridi kuwakabili TRA United

Simba SC yaingia ubaridi kuwakabili TRA United

 

WAKIWA kwenye maandalizi ya mwisho kuelelea mchezo wa NBC Premier League Simba SC vs TRA United, Machi 22, 2026 Uwanja wa Mej General Isahmuyo, wenyeji wameingiwa na ubaridi.

Simba SC imetoka Mwanza kwenye mji wenye mawe mengi na ziwa Victoria ambapo walikuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji FC.

Machi 19, 2026 ubao wa Kirumba ulisoma Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC wakigawana pointi mojamoja kwenye mchezo huo uliokamilika kwa jumla ya magoli mawili ndani ya dakika 90 na yote yalifungwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, amesema kuwa wanatambua wana mchezo mgumu dhidi ya TRA United hivyo wataingia kwa tahadhari kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Tunakwenda kwenye mchezo mgumu kuwakabili TRA United, hawa sio wapinzani wadogo kwani wana wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao tunapaswa kuwaangalia kwa umakini mkubwa.

“TRA United wana mchezaji mmoja anaitwa Chobwedo, ana kipara hivi akishachanganya ule upara unakuwa unatoa mvuke kama Chico vile ana hatari huyo, hivyo tupo tayari kwa mchezo wetu na tutawakabili wapinzani wagumu,”.

Msimamo wa Simba SC vs TRA United

POS

MP

W

D

L

PTS

3.Simba SC

13

8

4

1

28

10. TRA United

15

5

5

5

20

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.

Post a Comment

Previous Post Next Post