" MTIBWA SUGAR WAWAVURUGIA YANGA SC DAKIKA ZA MWISHO

MTIBWA SUGAR WAWAVURUGIA YANGA SC DAKIKA ZA MWISHO



Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamelazimishwa sare ya bao 1–1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa leo, Machi 21, 2026, katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Katika mchezo huo, wenyeji walisawazisha kipindi cha pili baada ya kuruhusu bao mapema kipindi cha kwanza ndani ya dakika 25.

Yanga SC walitangulia kufunga bao la ufunguzi dakika ya 23 ya mchezo kupitia kwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua, bao lililodumu hadi dakika ya 89.
Mtibwa Sugar walisawazisha bao dakika ya 90+2 kupitia kwa kiungo Ismael Mhesa katika muda wa nyongeza.

Kiungo huyo alianza kutoka benchi katika mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa, huku vinara Yanga SC wakishindwa kuvuna pointi tatu kwa mara ya tatu mfululizo.

Matokeo haya yanaifanya Yanga SC kufikisha jumla ya pointi 38 baada ya mechi 16, wakiendelea kuongoza ligi, huku Mtibwa Sugar wakiwa nafasi ya saba kwa pointi 22 baada ya mechi 16.

Post a Comment

Previous Post Next Post