Katibu wa Soko la Ngokolo Mitumbani.
Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media
Baadhi ya wajasiriamali wa soko la Ngokolo mitumbani Manispaa
ya Shinyanga wameeleza changamoto zinazowakabili na kuiomba serikali
kuwaboreshea miundombinu ya soko hilo ili kuwaepusha na usumbufu unaojitokeza.
Akizungumza na Misalaba Media katibu wa Soko hilo
Bwana Charles Bitengeko Machi 12, 2026 amesema wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali hasa katika kipindi cha masika ikiwemo maji kutuama
katika eneo la soko hilo na kusababisha aza kwa wajasiliamali na wananchi kwa
ujumla.
Bitegeko amesema kuwa changamoo hizo zimesababisha
upungufu wa wateja katika soko hilo na kuathiri ulipaji wa kodi kutokana na
kipato cha wajasiliamali kuwa kidogo.
Pia amesema changamoto ya maji kutuama inawaathiri pia
hadi akina mama wajasiliamali wa kupika chakula (Mama Ntilie) Pamoja na soko la
mbonga mboga lililopo hapo Ngokolo mitumbani.
Nao baadhi ya wajasiliamali wa Nguo za mitumba
wameeleza kuwa madibwi hayo yanasababisha mizigo inayoshushwa hapo kuchafuka
kutokana na maji au matope yaliyopo.
Hata hivyo wameita serikali kutatua changamoto
zinazowakabili kwani zimekuwa za muda mrefu na kwamba wamezifikisha kwa
viongozi husika lakini hazijapatiwa ufumbuzi hali inayoendelea kuwaathiri
wajasiliamali ikiwemo kushindwa kulipa kodi kwa wakati.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment