Katibu wa Soko la Ngokolo Mitumbani.Na Milu Malimi, Misalaba Media
Baadhi ya wajasiliamali wa soko la Ngokolo Mitumbani
katika Manispaa ya Shinyanga wametoa changamoto zinazowakabili kwenye soko hilo
hasa nyakati za mvua.
Wameeleza changamoto zao Machi 12, 2026 wakati
wakingumza na Misalaba Media ambapo wamesema changamoto hizo ni Pamoja na ubovu
wa miundombinu ya soko huku wakitaja uwepo wa mabonde yanayosababisha maji
mengi kutwama na kulete aza kwenye soko hilo.
Pia wajasiliamali hao wamesema walishawahi kuzifikisha
changamoto zao kwa viongozi wa serikali akiwemo mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga ambapo mpaka sasa hawajaona hatua zozote za kutatua changamoto hizo.
Hata hivyo katibu wa soko hilo Bwana Charles Betengeko
naye amesisitiza kuwa hivi karibuni walifanya mazungumza na kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo ambaye aliahidi kuzifanyia kazi.
Aidha katibu hiyo ameiomba serikali kupunguza kodi na
tozo kwa wajasiliamali hao kwani vinawaathiri kiuchumi kutokana na kwamba
haviendana na mapato ya biashara zao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment