
Moshi wafuka baada ya kombora la Israel kugonga makazi Beirut, Lebanon katika mashambulizi ya Amerika na Israel dhidi ya Hezbollah jana. Picha|Reuters
JESHI la Amerika lilitekeleza oparesheni ya kijasiri kumwokoa mwanajeshi wa anga aliyeachwa kwenye eneo la ‘adui’ baada ya Iran kuangusha ndege yake ya kivita, na kumsuluhishia Rais Donald Trump kitendawili kigumu, huku akitafakari kuendeleza mapigano yaliyo kwenye wiki yake ya sita sasa.
Afisa wa jeshi la angani aliyeokolewa na vikosi vya oparesheni maalumu, ambaye Trump alisema ni kanali, ni afisa wa silaha-mifumo kwenye ndege ya F-15 iliyoangushwa, afisa wa Amerika alieleza Reuters jana.
“Kwa saa kadhaa zilizopita, Jeshi la Amerika lilitekeleza moja kati ya Oparesheni hatari zaidi ua Msako na Uokoaji katika historia ya Amerika,” alisema Trump katika taarifa, akiongeza kuwa mwanajeshi huyo alijeruhiwa lakini “atakuwa sawa tu.”
Afisa huyo ni wa pili miongoni mwa maafisa wawili kwenue ndege ya kivita ambayo Iran ilisema Ijumaa iliangushwa na kikosi chake cha angani.
Jeshi la Iran lilisema ndege kadhaa ziliharibiwa wakati wa oparesheni ya uokoaji ya Amerika, kilirpoti kituo cha habari cha Tasnim.
Reuters iliripoti Ijumaa kwamba mwanajeshi wa kwanza ameokolewa na kusababisha msako mkali kutoka kwa Iran na Amerika kwa mwanajeshi aliyebaki.
Maafisa wa Iran waliwahimiza raia kuwasaidia kumpata, wakitumai kupata kisasi dhidi ya Washington kwenye vita vilivyoanzishwa na Trump na Israeli Februari 28.
Trump ametishia kuzidisha mapigano katika siku zijazo kwa kushambulia miundomsingi ya nishati Iran.
Endapo Iran ingemkamata mwanajeshi huyo wa angani, hali ambayo ingefuata ya kumshika mateka huenda ingebadilisha mtazamo wa Amerika kwa umma kuhusu vita ambavyo kura ya maoni tayari inaonyesha havina umaarufu.
Trump alisema mwanajeshi huyo wa kikosi cha anga aliokolewa “kwenye milima hatari ya Iran” kwenye kile alichosema ni mara ya kwanza kwa kumbukumbu za jeshi kuwa marubani wawili waliokolewa kandokando, ndani kabisa mwa eneo la adui.
Afisa huyo alieleza Reuters kwamba mwanajeshi huyo alipokuwa akisogeshwa kutoka karibu na mlima kwenye ndege ya usafiri iliyoegeshwa Iran, vikosi vya Amerika vililazimika kuharibu ndege moja kwa sababu ilikumbwa na hitilafu.
Juhudi za uokoaji zilizohusisha ndege kadhaa za kijeshi, zilikabiliwa na pingamizi kali kutoka Iran.
Reuters iliripoti Ijumaa kwamba helikopta mbili za Black Hawk zilizohusika kwenye msako huo zililengwa na Iran lakini zikatoweka kutoka anga la Iran.
Kando na tukio hilo, ruban aliyerushwa nje kutoka ndege ya kivita kwa jina A-10 Warthog iliyolengwa Kuwait na kuanguka, walisema maafisa, japo kiwango cha majeraha ya maafisa hakikubainika.
Hata hivyo, Trump alisherehekea ushindi.”
“Hali kwamba tunaweza kutekeleza oparesheni hizi mbili, pasipo raia hata mmoja wa Amerika kuuawa au hata kujeruhiwa, inathibitisha tu kwa mara nyingine, kwamba tumefanikisha kwa kiasi kikubwa Kutamalaki Angani na Mamlaka dhidi ya anga za Iran,” alisema katika taarifa yake.
Wanajeshi wa Amerika wamepokea mafunzo kuhusu wanachostahili kufanya iwapo wataangushwa na kusalia kwenye eneo a adui, mikakati inayofahamika kama Kujiokoa, Kukwepa, Kukataa na Kutoweka, lakini ni wachache wanazungumza Kiajemi kwa ufasaha na hukabiliwa na changamoto kukaa bila kugunduliwa wakitafuta kuokolewa.
Vita hivyo vimewaua wanajeshi 13 wa Amerika huku zaidi ya 300 kujeruhiwa, Mamkala ya Jeshi la Amerika inasema.
Hakuna vikosi vya Amerika vimeshikwa mateka na Iran
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment