" RC Makame: Atakayezua taharuki kupoteza ‘nyeti’ tutaruka naye

RC Makame: Atakayezua taharuki kupoteza ‘nyeti’ tutaruka naye

 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, leo Aprili 3, 2026 amefanya ziara maalum katika mji wa Tunduma kwa lengo la kutuliza taharuki iliyozuka miongoni mwa wananchi kufuatia madai ya vitendo vya wizi wa viungo vya uzazi kwa wanaume.

Akizungumza katika maeneo ya Kilimanjaro na Kisimani, Makame amelaani vikali vitendo hivyo na kusisitiza kuwa serikali haitavumilia uvunjifu wa amani wala vitendo vinavyochochea hofu kwa wananchi. Ameonya kuwa yeyote atakayezua taharuki au kuhusika na matukio hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema taarifa za hofu hiyo zimesababisha madhara makubwa, ikiwemo vifo na majeruhi, huku akisisitiza kuwa si jambo linalokubalika kwa wananchi kuishi kwa hofu katika eneo muhimu la kibiashara kama Tunduma.

Makame pia amekemea vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi vinavyochochewa na imani potofu, akieleza kuwa hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo na kuchafua taswira ya mkoa huo ambao ni lango muhimu la biashara.

Aidha, amewataka viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana na vyombo vya dola kudhibiti hali hiyo, huku akibainisha kuwa operesheni inaendelea kuwabaini wote wanaohusika.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga, amesema hadi sasa watu wanne wamepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa kutokana na matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi, huku watu 29 wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo.

Ametoa mfano wa tukio lililotokea Aprili 2, 2026 katika mji wa Vwawa, ambapo dereva wa bajaji alijeruhiwa baada ya mgogoro wa fedha uliogeuzwa kuwa tukio la madai ya kishirikina, na kusababisha kushambuliwa na wananchi

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post