" BIASHARA YA TANZANIA NA EU YAPAA KWA ASILIMIA 37.5 MWAKA 2025

BIASHARA YA TANZANIA NA EU YAPAA KWA ASILIMIA 37.5 MWAKA 2025

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Mei 22,2026 bungeni Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Biashara kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Ulaya imeendelea kuimarika mwaka 2025 huku mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko hilo yakiongezeka kwa kasi kubwa kutokana na kuimarika kwa ubora wa bidhaa pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za kikaboni.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026-2027,bungeni Waziri wa Viwanda na Biashara,Judith Kapinga,amesema mwaka 2025 inaonesha kuwa thamani ya bidhaa zilizouzwa na Tanzania kwenda nchi za Umoja wa Ulaya imefikia dola za Marekani milioni 943.8, ikilinganishwa na dola milioni 686.3 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 37.5.

Ongezeko hilo limechangiwa na juhudi za Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha viwango vya uzalishaji na kuongeza uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika soko la kimataifa.

Bidhaa zilizochangia zaidi ukuaji huo ni pamoja na maharage, tumbaku, samaki, parachichi, kahawa, kakao, asali, mafuta ya alizeti, chai, maua, matunda, mbogamboga, pamba, ngozi pamoja na vito vya thamani.

Katika upande mwingine, thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya imepungua kidogo mwaka 2025 na kufikia dola za Marekani milioni 1,260.13 kutoka dola milioni 1,267.6 mwaka 2024, sawa na upungufu wa asilimia 0.6.

Ameeleza kuwa upungufu huo umetokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani wa baadhi ya bidhaa zilizokuwa zikiagizwa kutoka nje, hususan mafuta ya kula, bidhaa za plastiki pamoja na baadhi ya vifaa vya msingi vya viwandani.

Bidhaa zinazoendelea kuagizwa kwa wingi kutoka Umoja wa Ulaya ni pamoja na mashine na mitambo ya viwandani, vifaa vya usafiri, kemikali, dawa za binadamu, vifaa vya umeme, mbolea pamoja na plastiki na bidhaa zake.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post