Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga Said Mankiligo ameipongeza ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 kwa kuendelea
kutoa nafasi kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 kushiriki mashindano
hayo huku akisema yanaendana na maelekezo na mwelekeo wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) katika kukuza vipaji vya vijana.
Akizungumza katika mashindano hayo yanayoendelea
kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Mankiligo amesema amefurahishwa na
namna waandaaji wa ligi hiyo walivyowapa nafasi kubwa vijana wadogo kuonesha
uwezo wao ndani ya uwanja.
Amesema mashindano hayo yana mchango mkubwa katika
kusaidia timu mbalimbali za Mkoa wa Shinyanga kupata nafasi ya kuona na
kuchagua wachezaji wenye vipaji badala ya kutegemea wachezaji wa gharama kubwa
wasiokidhi ushindani wa ligi mbalimbali.
Katika mchezo wa leo, timu ya NYANDOLWA imeibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya BAJAJI FC katika pambano lililojaa ushindani mkubwa
kwenye derby hiyo ya wachimbaji wa madini iliyochezwa katika uwanja wa
Mwabenda.
Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano
Sambayi Jilya ametangaza matokeo ya mchezo wa leo pamoja na kusoma ratiba ya
mechi ya kesho ambapo timu ya SHILABELA itamenyana na LYABUKANDE FC katika
mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya mashindano hayo.
Aidha amewakaribisha wananchi na wadau wa michezo
kuendelea kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo
hiyo ambayo imeendelea kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana kutoka maeneo
mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.
Ligi hiyo imeandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino
kupitia udhamini wa Lushu Foundation kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana,
kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kukuza michezo katika Mkoa wa
Shinyanga.
Mbali na kuwa mwandaaji wa mashindano ya NIACHEKONA
CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino ni mdau mkubwa wa michezo katika Wilaya ya
Shinyanga. Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja
na burudani unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0757 267 738.
Timu ya BAJAJI FC
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga Said Mankiligo akiwa katika zoezi la kukagua timu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga Said Mankiligo akiwa katika zoezi la kukagua timu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga Said Mankiligo akiwa katika zoezi la kukagua timu.
Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo wakifuatilia mchezo wa NYANDOLWA dhidi ya BAJAJI FC katika uwanja wa Mwabenda leo Mei 22, 2026.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



























Post a Comment