Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya DUARA FC imefanikiwa kutinga hatua inayofuata
ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya mpinzani wake MWANDUTU FC
kushindwa kufikia idadi ya mabao yaliyohitajika katika mchezo wa marudiano
uliochezwa kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga.
Katika mchezo wa leo Mei 29, 2026, timu hizo zimetoka
sare ya mabao 2-2 katika pambano lililokuwa na ushindani mkubwa huku mashabiki
wakishuhudia burudani ya hali ya juu ndani ya dakika 90 za mchezo.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo
ya mtoano, MWANDUTU FC walifungwa mabao 3-0 dhidi ya DUARA FC hali
iliyowalazimu kuhitaji ushindi mkubwa katika mchezo wa leo ili waweze kufuzu
hatua inayofuata.
Kutokana na sare ya mabao 2-2 ya leo, DUARA FC
imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2 kwa hesabu ya michezo yote
miwili ya marudiano.
Baada ya mchezo huo, viongozi wa MWANDUTU FC
wamemshukuru mwandaaji wa mashindano hayo Paul Daud Augustino kwa kuwapa nafasi
ya kushiriki katika mashindano hayo huku wakiahidi kurejea kwa nguvu zaidi
katika awamu zijazo za ligi hiyo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa mashindano ya
NIACHEKONA CUP Samwel Stephen ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo
SONGAMBELE MHANGU kutoka kata ya Salawe itamenyana na SHILIMA FC kutoka Mkoa wa
Mwanza katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Aidha amewahimiza wananchi pamoja na wadau wa michezo
kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kuendelea kushuhudia burudani ya
soka pamoja na vipaji vya vijana vinavyoendelea kuibuliwa kupitia mashindano
hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino kupitia ufadhili wa shirika la Lushu Foundation kwa lengo la
kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo pamoja na kuimarisha mshikamano wa
jamii kupitia soka.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali,
matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba
0757 267 738.
Kikosi cha Duara FC.
Wachezaji wa DUARA FC na MWANDUTU FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mchezo wa marudiano wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa leo Mei 29, 2026.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 Solwa.
Mchezo ukiendelea ambapo DUARA FC na MWANDUTU FC zilitoka sare ya mabao 2-2 katika pambano lililovutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya soka kupitia mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 Solwa.
Mashabiki wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa ushindani mkubwa kati ya DUARA FC na MWANDUTU FC katika uwanja wa Mwabenda.
Mashabiki wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa ushindani mkubwa kati ya DUARA FC na MWANDUTU FC katika uwanja wa Mwabenda.
Mashabiki wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo wa ushindani mkubwa kati ya DUARA FC na MWANDUTU FC katika uwanja wa Mwabenda.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment