" ISENENGEJA YAONESHA UKOMAVU DHIDI YA MWAKITOLYO No.6, SANGU FC NA BULIGE KUKIPIGA KESHO NIACHEKONA CUP

ISENENGEJA YAONESHA UKOMAVU DHIDI YA MWAKITOLYO No.6, SANGU FC NA BULIGE KUKIPIGA KESHO NIACHEKONA CUP


Na Mapuli Kitina Misalaba

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yameendelea kushika kasi ambapo timu ya ISENENGEJA imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MWAKITOLYO No.6 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi Jilya ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo timu ya SANGU FC itamenyana na BULIGE FC katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya ligi hiyo.

Aidha Sambayi ameendelea kuwahimiza wananchi wa jimbo la Solwa pamoja na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo hiyo ambayo imeendelea kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana kupitia soka.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino kupitia ufadhili wa Lushu Foundation kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo pamoja na kuimarisha mshikamano wa jamii kupitia soka.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja na burudani wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

ISENENGEJA FC 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post