" JAMB0 FM, MABULA LUSHU NA MISALABA MEDIA WAUNGA MKONO NIACHEKONA CUP

JAMB0 FM, MABULA LUSHU NA MISALABA MEDIA WAUNGA MKONO NIACHEKONA CUP

 

Na Mapuli Kitina Misalaba


Mdau wa michezo na mwandaaji wa mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Bwana Paul Daud Augustino amesema mashindano hayo yamelenga kuleta hamasa kubwa kwa vijana huku wadhamini mbalimbali wakitumia nafasi hiyo kutoa ujumbe wa maendeleo na kuwahimiza wananchi kujikita katika shughuli za uzalishaji mali.

Akizungumza katika muendelezo wa mashindano hayo yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, MC NIACHEKONA amesema wadhamini wake wameendelea kusimama bega kwa bega kuhakikisha ligi hiyo inafanikiwa huku ikibeba ujumbe wa kuwakutanisha vijana kupitia michezo.

Amesema mfadhili wake Mabula Lushu wa Mahembe ameendelea kutoa hamasa kwa vijana kwa kuwakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii kabla ya kujihusisha na burudani au vijiwe vya mazungumzo.

“Mabula Lushu anawakumbusha vijana kwamba maisha yanahitaji kazi kwanza. Kama wewe ni mkulima, mfugaji au mfanyabiashara hakikisha unatimiza majukumu yako kwa bidii ili uwe sehemu ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla,” amesema MC NIACHEKONA.

Ameongeza kuwa Mabula Lushu ambaye ni mkulima na mfugaji ameonesha dhamira ya kuwasaidia vijana kwa kutumia michezo kama sehemu ya kuwajenga na kuwaweka karibu na shughuli za maendeleo.

Aidha amesema mdhamini mwingine ambaye ni Jambo FM kupitia kipindi chake cha michezo ameendelea kuwafikishia wananchi taarifa mbalimbali kuhusu mwenendo wa mashindano hayo huku akiwahamasisha wananchi kuendelea kufuatilia vipindi vya michezo vinavyorushwa kila siku kuanzia saa moja na nusu.

“Jambo FM wanawakumbusha wananchi kuhakikisha wanaendelea kusikiliza vipindi vya michezo ili kupata taarifa mbalimbali za NIACHEKONA CUP pamoja na maendeleo ya ligi hii,” amesema.

Pia amesema Misalaba Media inaendelea kurusha matukio ya mashindano hayo kupitia majukwaa ya kidijitali ikiwemo YouTube na Instagram ambapo wananchi wamekuwa wakipata habari, matokeo na matukio mbalimbali ya michezo hiyo.

MC NIACHEKONA ameendelea kuwakaribisha wananchi wa Solwa na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kila siku kuanzia saa kumi jioni katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia burudani ya soka pamoja na vipaji vya vijana vinavyoendelea kuibuliwa kupitia mashindano hayo.

Mbali na kuwa mwandaaji wa mashindano hayo, Paul Daud Augustino ni mdau mkubwa wa michezo katika Wilaya ya Shinyanga ambaye amekuwa mstari wa mbele kusaidia timu mbalimbali pamoja na kuandaa mashindano ya vijana, huku NIACHEKONA CUP 2026 ikiwa ni ligi yake ya tatu kuandaa mwaka huu.

 

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, zikiwemo za kijamii na matukio tofauti wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.



 Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Mwabenda ambapo NYUNDO FC na NZOZA ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post