Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 inayoendelea katika uwanja
wa Mwabenda uliopo kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeendelea
kuvutia wadau mbalimbali wa michezo huku Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Shinyanga, Said Mankiligo akipongeza kiwango cha vipaji vinavyoendelea
kuonekana katika mashindano hayo.
Akizungumza baada ya kushuhudia baadhi ya michezo ya
ligi hiyo, Mankiligo amesema amefurahishwa na uwepo wa vijana wengi wenye
vipaji vya soka hususan wa umri wa chini ya miaka 20 ambao wanaendelea kuonesha
uwezo mkubwa ndani ya uwanja.
“Mimi nimefika katika kiwanja hiki kuja
kushuhudia mechi za ligi ya NIACHEKONA ambayo imeandaliwa na mdau wa michezo
Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA. Ukweli nimekuja kugundua kuna vipaji vingi vya
under 20 vinaonekana hapa, hii ndiyo fursa ya timu za Mkoa wa Shinyanga kuweza
kujua under 20 wako wapi kuliko kwenda kugharamikia kuchukua wachezaji wenye
majina makubwa ambao wakifika kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa wanaenda
kuenguliwa,” amesema Mankiligo.
Amesema viongozi wa vilabu vinavyoshiriki ligi ya Mkoa
wanapaswa kutumia mashindano hayo kama sehemu ya kusaka vipaji vya vijana
badala ya kutegemea wachezaji waliokwisha kupita katika kiwango cha ushindani.
“Kwahiyo nawashauri sana viongozi wa
vilabu vyote vya mpira ambavyo vitashiriki kwenye ligi ya Mkoa vifike katika
uwanja huu kuja kushuhudia na kujionea vipaji vilivyopo hapa. Nimekuja kugundua
vijana wenye vipaji vikubwa sana, wengi wao wana miaka 17, 18, 19 hadi 20 na
wakubwa ni wachache sana kwenye timu. Kwa kweli imenifurahisha sana,”
ameongeza.
Aidha amempongeza mwandaaji wa mashindano hayo Bwana
Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA kwa kuendelea kutoa nafasi kwa vijana kuonesha
vipaji vyao kupitia michezo huku akimtaka kuendelea kuandaa mashindano hayo
hata katika miaka ijayo.
Mankiligo pia ametoa wito kwa wadau wa michezo pamoja
na wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo ili kuendelea
kuwapa hamasa vijana wanaopambana kuonesha uwezo wao wa kisoka.
Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi
Jilya ametangaza matokeo ya mchezo wa leo ambapo timu ya SHILIMA kutoka Mkoa wa
Mwanza imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya SONGAMBELE MHANGU kutoka kata ya
Salawe katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Aidha amesema michezo itaendelea kesho ambapo NYUNDO
FC itashuka dimbani kuivaa NZOZA katika mchezo unaotarajiwa kuvuta mashabiki
wengi wa soka ndani na nje ya Solwa.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameshirikisha jumla
ya timu 22 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Geita, Kahama,
Manispaa ya Shinyanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la
kuibua vipaji vya vijana na kuimarisha mshikamano kupitia michezo.
Mpigie Bwana Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo na burudani unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0757 267 738.

Timu ya SONGAMBELE MHANGU
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga Said Mankiligo akisalimiana na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 kabla ya kuanza kwa mechi katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga Said Mankiligo akisalimiana na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 kabla ya kuanza kwa mechi katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga Said Mankiligo akisalimiana na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 kabla ya kuanza kwa mechi katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Wachezaji wa SHILIMA na SONGAMBELE MHANGU wakioneshana uwezo ndani ya dimba katika mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026
Wachezaji wa SHILIMA na SONGAMBELE MHANGU wakioneshana uwezo ndani ya dimba katika mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






























Post a Comment