" MANKILIGO AZIKUMBUSHA TIMU ZA NIACHEKONA CUP KUZINGATIA SHERIA ZA SOKA

MANKILIGO AZIKUMBUSHA TIMU ZA NIACHEKONA CUP KUZINGATIA SHERIA ZA SOKA


Na Mapuli Kitina Misalaba

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yameendelea kushika kasi ambapo mchezo wa leo Machi 21, 2026 uliwakutanisha MAHEMBE FC dhidi ya MAWEMIRU katika pambano lililovutia mashabiki waliojitokeza kushuhudia burudani ya soka.

Katika mchezo huo, MAHEMBE FC imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya MAWEMIRU baada ya kuonesha kiwango kizuri ndani ya dakika 90 za mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kuanzia kipindi cha kwanza hadi mwisho wa mchezo.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino kupitia udhamini na wadau mbalimbali ikiwemo Lushu Foundation kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na kuendeleza michezo katika Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga Said Mankiligo amezitaka timu pamoja na vijana wanaoshiriki mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha mashindano hayo yanaendelea kwa amani na ushindani wa haki.

Mankiligo amesema nidhamu ni msingi mkubwa wa mafanikio katika michezo hivyo wachezaji wanapaswa kuheshimu waamuzi, viongozi wa timu pamoja na mashabiki wakati wote wa mashindano hayo.

Aidha amewahimiza vijana kutumia mashindano hayo kama sehemu ya kuonesha vipaji vyao kwa njia ya nidhamu, mshikamano na kujituma ili waweze kuonekana na kupata nafasi katika timu mbalimbali za ngazi ya juu.

Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi Jilya ametangaza ratiba ya mechi ya derby kesho ambapo timu ya NYANDOLWA itashuka dimbani kumenyana na BAJAJ FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja wa Mwabenda.

Aidha amewakaribisha wananchi na wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hiyo ambayo imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji vya vijana kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Timu ya Mahembe FCTimu ya Mawemiru FC.Waamuzi wa mechi.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post