Mkoa wa Ruvuma umefanya harambe maalum ya wadau kuchangia watoto wa shule watakao shindana na kupata timu ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya kitaifa ya UMISSETA na UMITASHUMTA yatakayofanyika mkoani Iringa Harambe hiyo imefanya katika ukumbi wa chandamali uliopo manispaa ya songea ambao imewakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali,wakuu wa taasisi za serikali na binafsi Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma,mkuu wa wilaya ya Songea Mhe.kapenjama ndile amewataka wadau kuweza kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha wanaunga mkoni jitihada za mkoa na TAIFAAmesisitiza umuhimu wa michezo kama nyenzo ya ajira kwa vijana,kwani hii ni fursa ya kipekee kwa watoto hao kwenda kuonesha walichojaaliwaKwa upande wake katibu tawala mkoa wa Ruvuma Bi.mary makondo amesema lengo ni la harambe ni kuwashirikisha wadau wa maendeleo kuchangia watoto watakao kwenda kuuwakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa ya UMISSETA na UMITASHUMTA Amebainisha kuwa mkoa unataraji kupokea wanafunzi wa UMITASHUMTA 960 na walimu 112 ,na UMISSETA wanafunzi 960 na walimu 112 kwa siku 28 ambao mahitaji mbalimbali yatahitajika katika katika kambi hiyo ya kimkoa .Aidha ,kambi hiyo ya kimkoa inatarajiwa kuanza 23,May na kuwa na siku 28 za kutafuta timu moja ya kimkoa itakayokwenda kushiriki kitaifa mkoani Iringa
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment