Na Mapuli Kitina Misalaba
Ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 inayoendelea katika uwanja
wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeendelea
kushika kasi ambapo mchezo wa leo kati ya NYUNDO FC na NZOZA umemalizika kwa
sare ya bao 1-1 katika pambano lililokuwa na ushindani mkubwa na kuvutia
mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia burudani ya soka.
Mashindano hayo yanayoendelea kuibua vipaji vya vijana
kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga yameendelea kuwa
kivutio kikubwa kwa wadau wa michezo kutokana na ushindani wa timu pamoja na
mwitikio wa wananchi.
Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano
Sambayi Jilya ametangaza matokeo ya mchezo wa leo pamoja na kusoma ratiba ya
mechi ya kesho ambapo timu ya MAHEMBE itamenyana na MAWEMIRU katika mchezo
unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja wa Mwabenda.
Akiendelea kuzungumza, Sambayi amewakaribisha wananchi
na wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo hiyo ambayo
imeendelea kuwa jukwaa la kuibua vipaji vya vijana kutoka maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake mdau wa michezo Joseph Mbogo
amepongeza jitihada zinazofanywa na mwandaaji wa mashindano hayo Bwana Paul
Daud Augustino kwa namna anavyoendelea kutumia michezo kuwaunganisha vijana
pamoja na kuibua vipaji vyao.
Mbogo amesema NIACHEKONA CUP imekuwa chachu kubwa ya
maendeleo ya michezo katika kata ya Solwa na Wilaya ya Shinyanga kwa ujumla
kutokana na kuwapa vijana nafasi ya kuonesha uwezo wao mbele ya wadau
mbalimbali wa soka.
Aidha ameomba serikali kuendelea kumuunga mkono MC
NIACHEKONA katika juhudi zake za kuinua vipaji vya vijana kupitia michezo huku
akiiomba pia kuangalia nafasi inayoweza kumfaa katika sekta ya michezo iwe
ndani ya Wizara ya Michezo au Idara ya Michezo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga kutokana na mchango wake mkubwa anaouonesha kwa jamii kupitia
michezo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanaendelea kila siku kuanzia saa kumi jioni katika uwanja wa Mwabenda huku yakishirikisha jumla ya timu 22 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Geita, Kahama, Manispaa ya Shinyanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo, burudani, michezo, sherehe za kijamii na matukio tofauti wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
Nyundo FC kabla ya mechi.
Wachezaji wa NYUNDO FC na NZOZA wakioneshana uwezo katika mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026 uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Mwabenda ambapo NYUNDO FC na NZOZA ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Baadhi ya viongozi pamoja na wadau wa michezo wakifuatilia kwa karibu mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Wachezaji wakipambana kuwania mpira katika mchezo wa ushindani mkubwa wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa Solwa.
Wachezaji wakipambana kuwania mpira katika mchezo wa ushindani mkubwa wa NIACHEKONA CUP 2026 uliochezwa Solwa.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa hamasa mchezo wa NYUNDO FC dhidi ya NZOZA uliovutia mashabiki wengi.Mchezo ukiendelea katika uwanja wa Mwabenda ambapo NYUNDO FC na NZOZA ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1.







































Post a Comment