Wakulima wa zao la Ufuta wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameuza zao hilo kwa bei wastani wa tsh 2488 kwa kilo.Mnada huo ambao ni wa pili kufanyika katika msimu huu 2026/2027 umefanyika katika Kijiji Cha Lukumbule kupitia chama Cha msingi Nguvumali Amcos ambapo jumla ya kgs 228,403 za ufuta zimeuzwa katika mnada huoAkitangaza bei ya mnada huo Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu Tunduru Tamcu ndugu Kaisi Rashidi Makolela amesema bei ya juu katika mdao huo ni 2510 bei ya chini 2480 na bei wastani ni 2488 na wakulima wamekubali kuuza ufuta wao kwa bei hiyo.Kwa upande wao wakulima walioshiriki katika mnada huo wamesema bei inaridhisha lakin wameniomba Serikali pamoja na chama Kikuu Cha Ushirika Tunduru Tamcu kuwalipa kwa wakati wakulima ili waendelee na shughuli za kilimo ikiwemo upuliziaji wa zao la Korosho ambao unandelea hivi sasa.Nae diwani wa kata ya Lukumbule Mhe. Juma Makoka amepongeza namna minada inavyoendeshwa kwa kupitia mfumo wa kidijitali unaosimamiwa na TMX lakini ameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu ya namna minada ya sasa inavyoendeshwa ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza kutoka kwa wakulima ambao hawana uelewa mpana wa namna minada inavyoendeshwa kwa sasa.Kwa upande wao wakulima walioshiriki katika mnada huo wamesema bei hiyo ni nzuri lakini wameniomba Serikali pamoja na chama Kikuu Cha Ushirika Tunduru Tamcu kuwalipa wakulima kwa wakati ili waendelee na shughuli za kilimo ikiwemo upuliziaji wa zao la Korosho ambao unaondelea.lkumbukwe mnada wa kwanza wa ufuta msimu huu 2026/2027 uliofanyika kupitia Chama cha Msingi Mlingoti Mashariki bei wastani ilikuwa 2477 kwa kg ambapo pia mnada wa tatu unarajiwa kufanyika tarehe 02 /06/2026 katika Kijiji Cha kupitia chama Cha msingi Mtiti Amcos.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment