Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumia wakulima katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma (TAMCU Limited) kimefanikiwa kuuza kilo 994,681 za ufuta katika mnada wa kwanza wa msimu wa 2026/2027, huku bei ya juu ikiwa shilingi 2,520 kwa kilo na bei ya chini shilingi 2,410Mnada huo uliofanyika leo Mei 21, 2026 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru umehusisha wanunuzi sita walioshindana kununua mazao hayo kupitia lots 12, jambo lililoibua ushindani wa bei na kuongeza matumaini kwa wakulima.Takwimu za mnada huo zinaonesha kuwa bei ya kati ya ufuta imefikia shilingi 2,477 kwa kilo, hali inayotafsiriwa kuwa yenye manufaa kwa wakulima wa zao hilo wilayani Tunduru. Kiasi kikubwa cha ufuta kilichouzwa katika mnada wa kwanza kinaashiria kuendelea kuimarika kwa uzalishaji na biashara ya ufuta katika eneo hilo, huku mfumo wa minada ukiendelea kutoa fursa ya upatikanaji wa bei zenye ushindani.Mafanikio ya mnada huo yanatarajiwa kuongeza kipato kwa wakulima pamoja na kuimarisha uchumi wa kaya na Halmashauri kupitia biashara ya mazao ya kilimo. Wadau wa ushirika na kilimo wanaamini mwenendo wa bei katika minada ijayo unaweza kuendelea kuwapa motisha wakulima kuongeza uzalishaji wa ufuta kwa ubora unaohitajika sokoni.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment