Shirika la umeme Tanesco mkoa Ruvuma limeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufanya shughuli ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wateja katika Kata ya Madizini, Kitongoji cha Amka Twende, Halmashauri ya Songea Vijijini. Ziara hiyo imelenga kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kueleza changamoto zao moja kwa moja pamoja na kupata majibu na ufafanuzi wa kina kuhusu huduma wanazozihitaji.Akizungumza Afisa uhusiano huduma kwa wateja Allan Njiro amewahimiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwasilisha changamoto zao kwa wakati ili ziweze kupatiwa ufumbuzi mapema. Ameeleza kuwa lengo la kuwafuata wananchi katika maeneo yao ni kusogeza huduma karibu zaidi na jamii pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kati ya wananchi na taasisi zinazotoa huduma. Aidha, amesisitiza umuhimu wa mawasiliano mazuri katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.Kwa upande wao Wananchi wameeleza hatua ya viongozi kufika moja kwa moja katika maeneo yao imewapa nafasi ya kueleza changamoto zao kwa uwazi na kupata majibu yanayoridhisha. Wameeleza kuwa mikutano ya namna hiyo inasaidia kuongeza uelewa, kuimarisha ushirikiano na kujenga imani kati ya wananchi na watoa huduma katika jamii.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment