Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wamewataka Watanzania kuendelea kuliombea taifa ili liendelee kuwa salama na kuepukana na majanga pamoja na ajali mbalimbali zinazogharimu maisha ya wananchi nchini.
Wakizungumza na Misalaba Media leo Mei 21, 2026, ikiwa ni kumbukizi ya miaka 30 tangu kutokea kwa ajali ya meli ya MV Bukoba iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000, wananchi hao wameeleza umuhimu wa kuwakumbuka waliopoteza maisha katika ajali hiyo pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya majanga yanayoweza kuepukika.
Mmoja wa wananchi hao, Julius Joseph, amesema Watanzania wanapaswa kuungana katika maombi kwa ajili ya taifa kutokana na kuendelea kutokea kwa ajali mbalimbali zinazopoteza maisha ya mamia ya watu na kuacha huzuni kwa familia nyingi.
Ameeleza kuwa ajali hizo zimekuwa zikisababisha hofu na wasiwasi kwa wananchi wanaposafiri, hivyo kuna umuhimu wa kuchukua hatua za kuimarisha usalama katika sekta ya usafirishaji.
Kwa upande wake, Erick Nchuno amesema waendesha vyombo vya usafiri wanapaswa kuwa makini wanapotekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na majini, ikiwemo kuepuka kubeba mizigo au abiria kupita kiwango pamoja na kuendesha kwa mwendokasi.
Wananchi hao pia wameitaka serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza ajali zinazochangia vifo na ulemavu kwa wananchi, hali inayopunguza nguvu kazi ya taifa.
Aidha, wametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa ili kudumisha amani, mshikamano na usalama wa wananchi, wakisema maadili na hofu ya Mungu vina nafasi kubwa katika kujenga jamii yenye utulivu.
Hata hivyo, kumbukizi ya ajali ya meli ya MV Bukoba huadhimishwa kila mwaka Mei 21 katika eneo la Bwiru Igoma mkoani Mwanza, ambako kuna mnara wa kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment