" WAZIRI MKENDA SHERIA MPYA YA ELIMU IZINGATIE MASLAHI YA TAIFA

WAZIRI MKENDA SHERIA MPYA YA ELIMU IZINGATIE MASLAHI YA TAIFA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Caroline Nombo,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapitio ya Sheria y Elimu Wakili Frida Mwera ,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Mapitio ya Sheria ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wakili Innocent Mgeta ,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani)  katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani)  katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani)  katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea na jitihada za kuboresha Sheria ya Elimu ili iweze kuendana na mahitaji na mabadiliko ya sasa katika sekta ya elimu nchini.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Mei 21,2026 jijini Dodoma wakati akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353.
Prof Mkenda amesema  serikali imeendelea kufanya maboresho mbalimbali katika sekta ya elimu, ikiwemo kuandaa sera mpya, kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu nchini
 Amesema kuwa  tayari sera mpya ya elimu imezinduliwa na hatua inayofuata ni kufanya maboresho ya sheria ili kuendana na mwelekeo huo mpya wa elimu ifikapo mwaka 2028.
“Tunakutana kwa ajili ya kupitia mapendekezo ya sheria ambayo tayari yamefanyiwa kazi. Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 imefanyiwa marekebisho kadhaa, lakini sasa tunakusanya maoni yatakayosaidia kuamua kama tuje na sheria mpya au tufanye maboresho zaidi,” amesema Prof Mkenda.
Amesema  maoni yatakayokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa hatua zaidi za maamuzi.
Aidha,Prof.Mkenda amewashukuru wadau wa sekta ya elimu kwa ushiriki wao katika kutoa maoni na michango inayolenga kuboresha mfumo wa elimu nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir amesema kuwa  mchakato huo umechukua muda mrefu kwa lengo la kuhakikisha inapatikana sheria inayozingatia maoni ya wananchi wengi na wadau wa elimu.
"Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 imeweza kudumu kwa muda mrefu hivyo ipo haja ya wadau kutoa maoni yatakayosaidia kupatikana sheria bora itakayodumu kizazi hadi kizazi huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele."amesema Mhe.Wanu
Naye  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Caroline Nombo amesema  wizara imejipanga kuyachakata na kuyafanyia kazi maoni yote yatakayowasilishwa na wadau.
Hata hivyo amewataka washiriki kuwa wazi katika kutoa maoni yao ili kusaidia kupatikana kwa sheria bora yenye manufaa kwa taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post