" DC MKUDE APONGEZA UJIO WA CRDB BONGE LA WAKALA

DC MKUDE APONGEZA UJIO WA CRDB BONGE LA WAKALA


Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Joseph Mkude, ameipongeza Benki ya CRDB kuendelea kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini.Ameyasema hayo leo Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya CRDB Bonge la Wakala, akibainisha kuwa matumizi ya teknolojia yatasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi, kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kurahisisha shughuli za kiuchumi.Aidha amesema hatua hiyo inaendana na jitihada za Serikali za kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali, huku akiitaka benki hiyo kuendelea kubuni huduma bunifu zitakazowawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za kifedha kwa urahisi, usalama na kwa wakati. Hata hivyo amepongeza ongezeko la asilimia 98 ya huduma za benki kwa sasa zinazofanyika kupitia mifumo ya kidijitali, jambo linalorahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha na kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa urahisi na kwa wakati.DC  MKude amesema hatua hiyo inaunga mkono jitihada za kitaifa za kukuza uchumi wa kidijitali na maendeleo jumuishi, huku akiitaka CRDB kuendelea kupanua huduma zake na kuwekeza katika teknolojia bunifu zitakazosaidia kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika sekta ya fedha.Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda  ya kaskazini Emmanuel Kafui, amesema kupitia kampeni ya CRDB Bonge la Wakala, wateja watakaofanya miamala mbalimbali watapata fursa ya kujishindia fedha taslimu pamoja na zawadi tofauti kama sehemu ya kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha.Vilevile amesema benki hiyo inaendelea kupanua mtandao wa mawakala wake kwa kuhakikisha huduma zinapatikana katika maeneo mengi zaidi, ikiwemo vijijini, ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wakati.Mmoja wa Mawakala Hao Juliana Abraham amesema wapo tayari kuwahudumia wateja maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa kutoa elimu ya matumizi ya huduma za kifedha kwa ukaribu, ili kuongeza uelewa na kuwahamasisha wananchi kutumia huduma za benki kupitia mawakala waliopo karibu nao.Uzinduzi huo umebeba kauli mbiu "Bonge la Wakala Simu Bank Kimpango Wako".

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


 

Post a Comment

Previous Post Next Post