" DIWANI WA MWAWAZA AKUTANA NA WANANCHI, ASIKILIZA NA KUTATUA KERO MBALIMBALI

DIWANI WA MWAWAZA AKUTANA NA WANANCHI, ASIKILIZA NA KUTATUA KERO MBALIMBALI

Diwani wa Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, Edwin Charles Washa, leo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo kwa lengo la kuwashukuru kwa imani waliyoonyesha kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao, pamoja na kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Samwel Jackson.

Katika mkutano huo, wananchi walipata fursa ya kuwasilisha maoni, kero na mapendekezo yao kuhusu huduma mbalimbali za kijamii na maendeleo, huku viongozi waliokuwepo wakitoa majibu na ufafanuzi wa masuala yaliyoibuliwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Diwani Edwin Charles Washa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuonyesha na kuahidi kuendelea kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi wa Kata ya Mwawaza kwa kushirikiana na viongozi wa serikali na wadau wengine wa maendeleo.

Aidha, aliwahimiza wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kudumisha ushirikiano ili kuharakisha maendeleo ya kata hiyo na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Viongozi wengine ambao wamehudhuria mkutano huo ni Diwani wa Viti Maalumu tarafa ya Shinyanga mjini, Mwanahamisi Kazoba Mtendaji wa Kata ya Mwawaza, Naomi Stanley Kimaro Afisa Elimu wa Kata hiyo, Elizabeth Mboje Samweli Afisa Huduma kwa Wateja Masaka Kabesha, Mhandisi wa TARURA Eng. Kulwa Maige, pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Bwaga.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post