" HASSANI MSUMARI AONYA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

HASSANI MSUMARI AONYA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania, Hassan Msumari, ametoa mwito kwa jamii akieleza kuwa itakuwa ni aibu kubwa kwa kizazi cha sasa kuanza kuimomonyoa amani ya nchi waliyoirithi kutoka kwa viongozi waliotangulia.

 Akizungumza hivi karibuni kuhusu misingi ya uzalendo, Msumari amehimiza umuhimu wa Watanzania wote kuendelea kuilinda na kuienzi tunu hiyo muhimu ya taifa ili kuhakikisha utulivu unaendelea kutawala. 

Alibainisha kuwa Tanzania imekuwa ikijivunia kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye amani ya kudumu kutokana na juhudi za makusudi za viongozi waasisi na wananchi kwa ujumla waliojitoa kupambana katika kujenga misingi thabiti ya umoja, upendo, na mshikamano.

Kiongozi huyo wa chama cha Rhumba ameonya kuwa viashiria vidogo vinavyoonekana mtandaoni au kwenye jamii vinavyoweza kuchafua utulivu wa nchi havipaswi kubezwa hata kidogo, kwani mara nyingi migogoro mikubwa na ya umwagaji damu duniani huanza na mambo yanayoonekana madogo.

Amewataka wananchi kuifanya amani kuwa kipaumbele chao cha kwanza na kukubali kuwa mivutano ya kisiasa au kijamii inaweza kuwepo, lakini ni vyema kutumia uvumilivu na kutatua changamoto zote kwa njia ya mazungumzo yenye nia njema ya kulinda utulivu wa nchi yetu.

Akitolea mfano hali halisi ya duniani kwa sasa, Msumari amewatahadharisha Watanzania kuwa mataifa yenye uwezo wa kupokea na kuhifadhi wakimbizi yamepungua kwa kiasi kikubwa duniani.

 Alifafanua kuwa hata mataifa makubwa kama Marekani yamekuwa yakiwafukuza wakimbizi na kuwataka wale waliopo kurejea katika nchi zao huku wakisita kwa hofu, jambo linalopaswa kuwa funzo kubwa kwetu kutochafua nchi yetu. 

Kama mzalendo, ametoa ushauri wake wa mwisho akiwasihi wananchi wote kutochafua amani iliyopo bali kuendelea kuienzi na kuithamini Tanzania ili ibaki kuwa kimbilio salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post