" KASHISHI FC YAENDELEA KUANDIKA HISTORIA, YAMUONDOA KIGOGO MWINGINE SHILABELA FC KATIKA MASHINDANO YA NIACHEKONA CUP

KASHISHI FC YAENDELEA KUANDIKA HISTORIA, YAMUONDOA KIGOGO MWINGINE SHILABELA FC KATIKA MASHINDANO YA NIACHEKONA CUP

Na Mapuli Kitina Misalaba

Maajabu yameendelea kushuhudiwa katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya Kashishi FC kumuondoa kigogo mwingine, Shilabela FC, na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Kashishi FC, ambayo hivi karibuni ilimuondoa bingwa mtetezi wa mashindano hayo Sangu FC, leo Juni 16, 2026 imeendelea kuonyesha ubora wake baada ya kuitoa Shilabela FC, timu iliyowahi kufika fainali ya msimu wa 2024/2025 dhidi ya Sangu FC.

Mchezo huo wa robo fainali uliochezwa katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, umemalizika kwa sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyozilazimu timu hizo kwenda katika hatua ya mikwaju ya penati kutafuta mshindi.

Katika mikwaju hiyo ya penati, Kashishi FC ilionyesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kupata penati 4 kwa 3, matokeo yaliyoihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali huku safari ya Shilabela FC ikifikia tamati.

Kwa ushindi huo, Kashishi FC imejiwekea rekodi ya kuwa miongoni mwa timu zilizofanya makubwa zaidi katika mashindano ya mwaka huu baada ya kuwaondoa vigogo wawili mfululizo waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufika fainali.

Hatua ya nusu fainali sasa itawakutanisha Kashishi FC dhidi ya Bulige FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kiwango walichoonyesha timu hizo katika hatua zilizopita.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP, Sambayi Jilya, amesema kuwa kesho Jumatano kutakuwa na mapumziko ili kutoa nafasi kwa maandalizi ya hatua ya nusu fainali.

Amesema mchezo wa kwanza wa nusu fainali utachezwa Alhamisi, Juni 18, ambapo Ufukunyungu FC itamenyana na Duara FC, huku mchezo wa pili wa nusu fainali ukiwakutanisha Bulige FC na Kashishi FC siku ya Juni 19.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Kikosi cha Shilabela FC.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post