" MC NIACHEKONA: FAINALI YA NIACHEKONA CUP 2026 ITAKUWA YA KIHISTORIA

MC NIACHEKONA: FAINALI YA NIACHEKONA CUP 2026 ITAKUWA YA KIHISTORIA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkurugenzi wa mashindano ya NIACHEKONA CUP, Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA, amewashukuru Watanzania, wadau wa michezo na timu zote zilizoshiriki mashindano hayo kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu pamoja na nidhamu tangu kuanza kwa michuano hiyo hadi kufikia hatua ya fainali.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa michezo ya nusu fainali, MC NIACHEKONA amesema timu zilizofanikiwa kutinga fainali ni Ufukunyungu FC kutoka Manispaa ya Shinyanga na Kashishi FC kutoka Kata ya Solwa, huku akieleza kufurahishwa na kiwango na nidhamu iliyoonyeshwa na washiriki wa mashindano hayo.

"Ninawashukuru Watanzania wote na timu zote zilizoshiriki katika mashindano haya. Mmeonyesha mpira mzuri na nidhamu ya hali ya juu tangu tulipoanza hadi tumefikia hatua hii ya fainali," amesema NIACHEKONA.

Ametumia nafasi hiyo kuwaalika wananchi na wadau mbalimbali wa michezo kuhudhuria mchezo wa fainali utakaofanyika Jumanne, Juni 23, 2026, katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa.

Amesema siku hiyo mchezo wa kusaka mshindi wa tatu utaanza saa nane mchana, huku saa kumi kamili kukiwa na hotuba ya mgeni rasmi ambaye atatangazwa rasmi siku ya Jumatatu kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali.

"Ninawaalika Watanzania wote kuhudhuria fainali hii. Kutakuwa na burudani mbalimbali na shughuli nyingi za kuvutia kwa mashabiki na wananchi wote watakaohudhuria," ameongeza.

MC NIACHEKONA pia amewashukuru wadau mbalimbali waliochangia mafanikio ya mashindano hayo, akilitaja Shirika la Lushu Foundation kwa kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa mashindano pamoja na Misalaba Media kwa kazi ya kuripoti na kusambaza taarifa za mashindano kwa wananchi kupitia vyombo na mitandao ya kijamii.

Aidha, amesema yupo tayari kushirikiana na wadau wote wa michezo wanaotaka kuendeleza vipaji na kukuza michezo nchini kutokana na uzoefu alioupata katika kuandaa na kusimamia mashindano mbalimbali.

Kumbuka huu ni msimu wa tatau wa Mashindano ya NIACHEKONA CUP  ambayo yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA na kwambwa msimu huu yamefadhiliwa na Shirika la Lushu Foundation, ikiwa lengo ni kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post