" UFUKUNYUNGU FC YATINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUMUONDOA (KIGOGO) SONGAMBELE MHANGU FC

UFUKUNYUNGU FC YATINGA NUSU FAINALI BAADA YA KUMUONDOA (KIGOGO) SONGAMBELE MHANGU FC


Na Mapuli Kitina Misalaba

Timu ya Ufukunyungu FC imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Songambele Mhangu FC katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa leo Juni 13, 2026 katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa Ufukunyungu FC kupata bao pekee la ushindi katika kipindi cha pili kupitia mshambuliaji wake Said Saidi, ambaye aliandika historia ya kuipa timu yake tiketi ya kutinga hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo, huku Songambele Mhangu FC ikishindwa kupata bao la kusawazisha licha ya kufanya juhudi mbalimbali mbele ya lango la wapinzani wao.

Kwa ushindi huo, Ufukunyungu FC imefanikiwa kumuondoa mmoja wa vigogo waliokuwa wakitajwa kuwania ubingwa wa NIACHEKONA CUP 2026. Songambele Mhangu FC ilikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na historia yake nzuri katika mashindano mbalimbali pamoja na kuwa na wadhamini waliokuwa wakiiwezesha timu hiyo.

Baada ya mchezo huo, mashabiki na wadau wa michezo wamepongeza kiwango kilichooneshwa na timu zote mbili huku wakieleza kuwa ushindi wa Ufukunyungu FC umeongeza ushindani katika hatua ya nusu fainali.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP, Sambayi Jilya, ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho ambapo Duara FC itamenyana na Mawemiru FC katika mchezo mwingine wa robo fainali utakaochezwa katika Uwanja wa Mwabenda.

Sambayi Jilya amewahimiza wananchi, mashabiki na wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezo iliyosalia katika hatua ya robo fainali.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa huduma za MC, matangazo na usimamizi wa matukio mbalimbali ya kijamii, wasiliana na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Kikosi cha Songambele Mhangu FC.


 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post