" WANANCHI MSIKUBALI MANENO YA USHAWISHI; WAKOMALIENI WACHOCHEZI

WANANCHI MSIKUBALI MANENO YA USHAWISHI; WAKOMALIENI WACHOCHEZI



Wananchi na vijana kote nchini wanahimizwa kuwa macho na kutokubali kabisa kuyasikiliza maneno ya ushawishi yanayohubiri chuki na uharibifu.Badala yake, jamii inatakiwa kushikamana na "kuwakomalia" kikamilifu watu wote wanaojaribu kupandikiza mbegu za machafuko, iwe ni mitaani au kwenye mitandao ya kijamii.



Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Laban Kihongosi, alisisitiza kuwa kulinda amani ni wajibu wa kila mmoja:


"Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa salama, yenye amani na utulivu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho."


Aidha wananchi wametakiwa kuwa na Kumbukumbu za matukio ya nyuma, hususan Oktoba 29, ambayo yanasalia kuwa funzo kubwa na la kudumu kwa Watanzania wote.


Historia inatufundisha kuwa ghasia, vurugu, na uharibifu wa mali wakati wa harakati za kisiasa haujawahi kuleta tija, bali huacha makovu yasiyofutika, vifo, ulemavu, na kuporomoka kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


Wananchi wanatakiwa kukumbuka machungu ya nyuma na kukataa katakata kutumika kama kuni za kuwasha moto utakaoteketeza nchi yao wenyewe.


Kauli hioyo imetolewa huku upande wa upinzani kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ukilalamikia misukosuko ya kisheria na kiutawala


Wadau wa amani wanasisitiza kuwa madai yoyote ya kisiasa lazima yafuate njia za kisheria na amani, bila kuingiza nchi kwenye dimbwi la damu na moto.


Siri nzito imevuja kuhusu uwepo wa mikakati ya kisiri inayoratibiwa na baadhi ya watu wenye nia ovu, inayolenga kutumia mwavuli wa maandamano na mikutano kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umma, ikiwemo kuchoma moto shule na vyuo.


Taarifa za kiintelijensia na vyanzo vya kuaminika vinabainisha kuwa, baadhi ya vikundi na akaunti za mitandao ya kijamii zinazoendeshwa na watu wenye msimamo mkali—akiwemo mchochezi anayejulikana zimekuwa zikisuka mipango hiyo hatari kwa lengo la kuleta taharuki, kuvuruga usalama, na kuifanya nchi isitawalike.


Wachambuzi wa masuala ya usalama na maendeleo wameonya vikali dhidi ya fikra hizi za kiharifu. Swali kubwa linaloulizwa na kila Mtanzania mzalendo ni: "Ukishachoma nchi moto, ukaharibu shule na vyuo vinavyolelea watoto wetu, unatarajia kupata nini?"


Kuchoma shule na vyuo siyo kupigania demokrasia, bali ni kuharibu mustakabali wa elimu ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kitendo cha kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa kodi za Watanzania maskini ni kujirudisha nyuma kimaendeleo na kuongeza umaskini. Maisha ya wananchi yakishaharibika na amani ikitoweka, hakuna mshindi—sote tutakuwa waathirika.


"Maendeleo ya haraka yaliyopatikana Tanzania Bara na Zanzibar yametokana na kuwepo kwa amani na utulivu. Vijana wa Kitanzania msikubali kuiweka nchi yenu rehani," alikaririwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar (Itikadi na Uenezi), Khamisi Mbeto Khamis, akionya dhidi ya maandamano haramu.


Amewataka watanzania kulinda shule yako, linda chuo chako, na kemea kila sauti inayohamasisha uharibifu. Tanzania ni yetu sote, na kuichoma moto ni kujiteketeza wenyewe.

Post a Comment

Previous Post Next Post