Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo wilayani Msalala Mkoani Shinyanga umeendelea na kampeni yake ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria ijulikanayo kama “Zero Malaria” kwa kuwezesha kupuliza dawa kwenye mazalia ya mbu na majumbani kwenye kaya zipatazo 44,000 zilizopo kwenye kata za Bugarama na Bulyanhulu.Akizungumza baada ya kuhitimisha zoezi ambako limepongezwa na wananchi wengi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala ambaye ni mratibu wa kupambana na wadudu wadhulifu ngazi ya wilaya , Julieth Petro amesema kwamba zoezi hilo limefanikiwa kufikia hizo kaya zilizopo kwenye kata mbili.Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umekuwa ukiwezesha shughuli mbalimbali za kijamii , ikiwa ni pamoja na afua za afya kama vile upuliziaji wa dawa za mbu majumbani (Indoor Residual Spraying- IRS) ili kupambana na malari katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.Akiongelea kampeni hiyo Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu , Zuwena Senkondo amesema lengo la zoezi hilo ni kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa kuua na kutokomeza mazalia ya mbu kwenye kaya zilizopo karibu na mgodi na limekuwa likifanyika kila mwaka.Senkondo amesema kuwa Barrick Bulyanhulu itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi sambamba na kuhakikisha wanakuwa na afya bora.“Afya ni suala la muhimu katika jamii yoyote ile ndio maana Barrick Bulyanhulu tumekuja na kampeni ya kutokomeza ugonjwa hatari wa Malaria ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa huu na nina imani sote tukiungana pamoja tutafanikiwa kutokomeza ugonjwa huu” alisema Senkondo.Senkondo alifafanua kwamba kupitia kampeni hii ya awamu ya kwanza mwaka huu , imeweza kuzifikia kaya elfu 44 katika makazi yao kwa kunyunyiziwa dawa za kuua mazalia ya mbu sambamba kugawiwa wananchi vyandarua .Pamoja na mambo mengine alisisitiza kwamba aina ya dawa zinazotumika ni salama na zimeidhinishwa kwa matumizi ya nyumbani kama vile (Pyrethroids) na ufadhili huo unalenga kwenye vijiji na jamii inavyozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu.Zoezi hilo la Upuliziaji wa liliendeshwa na kampuni ya Gekahil Inter - Trade ltd huku vijana takribani 95 walipata ajira za muda baada ya kushiriki zoezi hilo la zero malaria kampuni yenye kauli mbiu “Zero Malaria Inaanza na mimi , wewe na sisi sote”Mpango huu wa kupuliza dawa za kuua mbu, kugawa vyandarua vyenye dawa bure kwa wafanyakazi na jamii , utoaji wa elimu na kuhamasisha upimaji afya wa mara kwa mara umefanikisha kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria katika kata zinazozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu Mwisho
Jullieth Petro (Katikati) - Mratibu wa Wadudu wadhulifu Ngazi ya wilaya akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Msalala akitoa cheti kwa mmoja ya washiriki wa zoezi la kupuliza dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu katika zoezi la kupambana na ugonjwa wa malaria ambao ni mradi wa Barrick Bulyanhulu wa “Zero Malaria’ kushoto kabisa ni Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu , Zuwena SenkondoSHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment