Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, Mwl. Vumilia Julius Simbeye amesema Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mpango wa kuwaandikisha shule watoto wote waliofikia umri wa kuanza shule wakiwemo watoto wenye ulemavu wa akili ili kuhakikisha wanapata haki yao ya msingi ya kupata elimu. Mwl. Simbeye ameyasema hayo wakati akifunga Bonanza Maalumu la Michezo kwa Watoto Wenye Ulemavu wa akili lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nyumbigwa, ambapo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha usawa na ujumuishwaji katika kutoa huduma za kijamii. Aidha, ametoa wito kwa jamii kuachana na mitazamo potofu dhidi ya watoto wenye ulemavu wa akili akieleza kuwa Serikali inawatambua, inawajali na inathamini mchango wa kila mtoto na itaendelea kuhakikisha wanapata haki na fursa stahiki katika nyanja mbalimbali za maisha.Kwa upande wao, wazazi na walezi wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa watoto wenye ulemavu huo huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto hao wanapata elimu, malezi bora na fursa sawa za maendeleo. Kwa upande wao, watoto wameeleza furaha yao kwa kupata nafasi ya kushiriki katika michezo wakitoa wito kwa jamii kuwatambua, kuwajali na kuwapa fursa sawa ili waweze kuonyesha uwezo na vipaji walivyonavyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, Mwl. Vumilia Julius Simbeye akizungumza.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment