" WAZIRI MKUU MWIGULU NA UWT WASHIRIKIANA KUCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU BMH

WAZIRI MKUU MWIGULU NA UWT WASHIRIKIANA KUCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU BMH


NA: MWANDISHI WETU, DODOMAWaziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ameshiriki hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwezesha Mfuko wa Gharama za Matibabu kwa Wagonjwa wa Figo na Upandikizaji Uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).Hafla hiyo imefanyika Julai 16, 2026, katika Ukumbi wa Mabele Mabeyo Jijini Dodoma, ambapo Dk. Mwigulu amesema, jambo hilo ni jema kwani linawezesha kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa wasio na uwezo wa kugharamia matibabu hayo."Tunachokifanya leo ni kurejesha matumaini kwa wagonjwa na familia zao. Kila anayeguswa na jambo hili aendelee kushiriki ili wananchi wengi zaidi wanufaike na huduma hizi muhimu," amesema Dk. Mwigulu.Aidha, amesema serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza fedha nyingi ili kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.Naye, Wazi wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema, dhamira ya serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha huduma bora za kibingwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda amesema, UWT inaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya ambapo imesaidia sana kuokoa maisha ya wananchi na ndiyo maana wamehamasishana kuchangia fedha."UWT tuko pamoja na serikali yetu, na hapa niseme, linapokuja suala la maendeleo kama hili la kuboresha sekta ya afya, tunakuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kufanikisha," amesema Chatanda.Katika tukio hilo la aina yake na la kihistoria, limewakutanisha viongozi mbalimbali wa kisiasa, dini, taasisi, wadau, na wananchi. Aidha, fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.225 zimepatikana, huku wananchi wakihamasishwa kuendelea kuchangia kwani jambo hilo ni endelevu.Kimsingi, Hospitali ya Benjamin Mkapa imetimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, ambapo mkakati wake ni kukusanya shilingi bilioni saba za mfuko wa kugharamia matibabu ya magonjwa figo na upandikizaji uloto.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



 

Post a Comment

Previous Post Next Post