

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa, tarehe 18 Julai Juni, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi wakati wakupokea heshima ya wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Misri baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akikagua Gwaride rasmi la Mapokezi lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mheshimiwa Abdel Fattah El-Sisi, aliyewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku moja.
Post a Comment