Na Mapuli Kitina Misalaba
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, tawi
la Tanzania (MISA Tanzania), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma
za Nishati na Maji (EWURA), imeendesha warsha ya tathmini ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari na wahariri, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya
mafunzo yaliyofanyika Juni 16, 2025.
Akizungumza katika warsha hiyo leo Februari 27, 2026 jijini Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa MISA TAN, Edwin Soko, ameishukuru EWURA kwa kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo katika kuwawezesha waandishi wa habari kuandika
kwa weledi kuhusu masuala ya uthibiti wa nishati na maji.
Amesema tangu mafunzo ya awali kufanyika, jumla ya
habari 103 zimeandikwa na kurushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, hatua
inayodhihirisha mafanikio ya ushirikiano huo.
Ameongeza kuwa MISA TAN inaishukuru EWURA kwa
kuwaamini na kuahidi kuwa waandishi waliopata mafunzo wataendelea kuwa mabalozi
wazuri wa taasisi hiyo popote walipo.
Katika wasilisho lake, Mwenyekiti huyo amesisitiza
matarajio ya kuona habari zenye weledi, zinazozingatia maadili ya taaluma na
zenye kuleta suluhisho kwa jamii huku akiwasisitiza washiriki kuendelea
kuandika kwa ufasaha kuhusu majukumu ya EWURA baada ya kuifahamu vyema mamlaka
hiyo, pamoja na kufanya kazi kwa karibu na ofisi za kanda za EWURA ili kupata
taarifa sahihi.
Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lorivii
Long’idu, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA amesema jukumu la
EWURA ni kuelimisha umma kuhusu masuala ya uthibiti wa huduma za nishati na
maji, na kwamba kupitia vyombo vya habari wanaamini wakielimisha waandishi wa
habari wanakuwa wameuelimisha umma kwa ujumla.
Ameeleza kuwa katika sekta ya nishati, kwa takwimu
zilizopo nchini, huduma zinaendelea vizuri na ubora wake umeimarika ambapo amewaomba
waandishi kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa kuandika habari za kuelimisha umma
kwa kuzingatia maadili na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari.
Aidha, amebainisha kuwa EWURA imekuwa ikitoa
ushirikiano kwa waandishi wa habari na itaendelea kufanya hivyo, ili
kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu haki na wajibu wao katika
matumizi ya huduma za nishati na maji.
Kuhusu changamoto zilizopo, amesema baadhi ya
watumiaji wa huduma hizo wamekuwa na mazoea yanayochangia malalamiko yasiyo
rasmi, akiwataka waandishi kusaidia kuelimisha wananchi kuchukua hatua stahiki
kwa kufikisha malalamiko yao katika ofisi za EWURA.
Ametolea mfano changamoto zinazowakabili baadhi ya
wamiliki wa magari wakati wa kununua mafuta, pamoja na bili bandikizi za maji
au umeme, akisisitiza kuwa malalamiko hayo yakifikishwa katika ofisi za EWURA
hushughulikiwa bila gharama yoyote.
Mhandisi Long’idu amesisitiza kuwa EWURA itaendelea
kushirikiana na vyombo vya habari katika juhudi za kuwafikishia wananchi elimu
juu ya wajibu wao na namna bora ya kunufaika na huduma za nishati na maji.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wilfred Mwakalosi,
amesema bado wananchi wengi hawafahamu haki na wajibu wao katika huduma za
nishati na maji, hali inayochangia baadhi yao kushindwa kudai haki zao au
kutotimiza wajibu wao ipasavyo.
Amesema uelewa mdogo kwa wananchi unasababisha
malalamiko mengi kutowasilishwa katika mamlaka husika kwa wakati, huku wengine
wakishindwa kufuata taratibu sahihi za kupata huduma au kuwasilisha changamoto
zao.
Ameongeza kuwa wananchi wakifahamu haki zao pamoja na
wajibu wao, itasaidia watoa huduma kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kwa
ufanisi zaidi, sambamba na kuimarisha uwajibikaji katika sekta ya nishati na
maji.
Warsha hiyo imehusisha majadiliano ya wazi, maswali na
majibu kati ya washiriki na wataalamu wa EWURA, pamoja na kufikiwa kwa maazimio
ya pamoja yaliyolenga kuimarisha uandishi wa habari za sekta ya nishati na maji
kwa weledi na uwajibikaji. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi
endelevu za kuimarisha ushirikiano kati ya MISA Tanzania na Mamlaka ya Udhibiti
wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa lengo la kuhakikisha wananchi
wanapata taarifa sahihi, zenye kuelimisha na kuchochea uwajibikaji katika
matumizi ya huduma za nishati na maji.
Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lorivii Long’idu,
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA
Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lorivii Long’idu,
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA
Mwenyekiti wa MISA TAN, Edwin Soko, akiishukuru EWURA kwa kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa MISA TAN, Edwin Soko, akiishukuru EWURA kwa kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo. 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






































































Post a Comment