Na Lydia Lugakila- Misalaba MediaMbeyaKatika kuadhimisha Wiki ya Maji, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWSA), kwa kushirikiana na watumishi wake pamoja na waandishi wa habari, imefanya ziara maalum ya kutembelea mradi wa kimkakati uliopo eneo la Forest Mpya jijini Mbeya.Ziara hiyo imelenga kujionea hatua za utekelezaji wa mradi wa maji wa mto Kiwira, ambao ni miongoni mwa miradi muhimu inayolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa jiji hilo.Katika mradi huo, kazi kubwa inaendelea, ikiwemo ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni tano za maji kwa siku.Hadi sasa, ujenzi huo umefikia asilimia 62, hatua inayoashiria maendeleo mazuri ya utekelezaji wake.Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Barnabas Konga, amesema kuwa ndani ya wiki hii wanatarajia kuanza hatua muhimu ya kumwaga zege kwa siku tatu mfululizo, ili kukamilisha sehemu muhimu ya ujenzi wa tenki hilo.Katika kuhitimisha ziara hiyo, Mhandisi Konga ameeleza kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika, ikiwa ni pamoja na usukaji wa nondo unaoonekana tayari katika eneo la mradi.Hali hiyo inaonyesha utayari wa kuendelea na hatua zinazofuata kwa kasi zaidi ambapo pia amesisitiza kuwa mafanikio ya mradi huo yatachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya maji safi kwa wakazi wa Mbeya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment