Gari la Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga limepata ajali eneo la Usanda wilaya ya Shinyanga barabara ya Tabora - Shinyanga, wakati likikwepa gari aina ya Toyota Harrier na kuingia kwenye mtaro.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa watu watano wamejeruhiwa katika ajali hiyo akiwemo Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One Bw. Frank Mshana, Johnson Zacharia na Boazi.
Majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Taarifa zaidi zitawajia kadiri tutakavyo zipata.

CHANZO - ITV
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment