Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Isaac Antony Mwakisu amempongeza Mkurugenzi wa Mji Kasulu na timu ya wataalamu kwa usimamiaji mzuri wa miradi ya maendeleo.Ameyasema hayo wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) Wilaya ya Kasulu ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kasange wenye gharama ya shilingi milioni 342,900,000 ambao ni maandalizi ya mapokezi ya mtaala mpya wa elimu ya msingi unaoanzia awali mpaka kidato cha nne.Aidha, Kanali Mwakisu amesisitiza kufanya marekebisho machache yaliyosalia na kuwataka wataalamu kusimamia miradi kwa maelekezo yaliyotolewa ikiwemo kuzingatia BoQ na ramani kama ilivyoelekezwa pamoja na ufuatiliaji wa viwanja kuwa na hati. Ameeleza kuwa usimamizi mzuri wa miradi ndio huleta ufanisi, ikiwemo mradi kutumika kwa muda mrefu na wananchi.Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa madarasa na vyoo katika Shule ya Msingi Bwami, ujenzi wa shule ya wenye mahitaji maalumu Kabanga mazoezi, ukumbi wa sherehe na mikutano pamoja na nyumba ya Mkurugenzi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


















Post a Comment