Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Hamad Masauni amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kuwapa watoto elimu ya mazingira ili kusaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi zinazoendelea kuathiri dunia.Amezungumza hayo Jijini Arusha katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira duniani na kusisitiza kuwa mazingira bora ni msingi wa maisha ya binadamu na maendeleo ya taifa, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha anashiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.Aidha Waziri Masauni amesema kuwa elimu ya mazingira ianze kutolewa kwa watoto tangu wakiwa wadogo ili kujenga jamii yenye uelewa mkubwa wa kutunza mazingira.Sambamba na hayo amehimiza matumizi ya nishati safi akisema matumizi hayo yatasaidia kupunguza gharama za maisha, kuokoa muda na kupunguza hewa ukaa inayochangia ongezeko la joto duniani."Matumizi ya nishati safi ni hatua muhimu katika kulinda afya za wananchi na mazingira kwa ujumla, serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia na nishati mbadala rafiki kwa mazingira ili kuhakikisha wananchi wanaachana na matumizi ya nishati zinazochangia uharibifu wa mazingira na ukataji holela wa miti.Vile vile Waziri Masauni ameshiriki upandaji wa miti ya matunda na kugawa miti kwa wananfunzi shule ya sekondari Arusha, ambapo pia ameridhishwa na mradi wa nishati safi shuleni hapo unaosaidia kuandaa chakula Kwa wanafunzi hao.Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt.Toba Nguvila Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amesema suala la utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi linapaswa kupewa kipaumbele na kila mwananchi."Mkoa wa Arusha unaendelea kuongoza kwa usafi nchini kutokana na juhudi za wananchi na viongozi wake katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama wakati wote. Ni wajibu wa kila mmoja kuendelea kulinda hadhi hiyo kwa kutunza mazingira"amesema.Pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kupanda miti kwa wingi kama sehemu ya kuhifadhi mazingira na kuacha urithi mzuri kwa vizazi vijavyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Hamad Masauni, akipanda mti.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment